Friday , 29 September 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Jafo: Uandikishaji wapiga kura Serikali za Mitaa, wavunja rekodi
Habari za Siasa

Jafo: Uandikishaji wapiga kura Serikali za Mitaa, wavunja rekodi

Suleiman Jafo, Waziri wa Tamisemi
Spread the love

ZOEZI la uandikishaji wa daftari la wa wapiga kura wa uchaguzi wa serikali za mitaa kwa mwaka 2019 umevunja rekodi tofauti na miaka iliyopita huku wakiandikishwa zaidi ya watu milioni 19.6 sawa na asilimia 86. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma … (endelea).

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Selemani Jafo amesema hayo wakati akitoa tathimini ya zoezi la uandikishaji kwa waandishi wa habari ofisini kwake katika eneo la Mtumba jijini Dodoma.

Alibainisha kuwa kwa mujibu wa makadirio ya wapiga kura iliyotolewa na ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), wananchi wenye sifa ya kupiga kura ni wenye umri miaka 18.

Alisema katika uchaguzi huu wa serikali za mitaa wa mwaka 2019 wanakadiriwa kufikia milioni 26.9 ambapo kati yao wanaume ni milioni 12.8 na wanawake ni milioni 14.1.

Jafo alisema wakati alipotangaza kipyenga cha uchaguzi walikadiria kuandikisha wapiga kura milioni 22 ambao ni sawa na asilimia 85 ya wananchi wenye sifa za kupiga kura ambapo wanaume ni milioni 10.9 na wanawake milioni 11.9.

Alisema kuwa hadi juzi jumla ya wapiga kura milioni 19.6 wamejiandikisha katika daftari la orodha ya wapiga kura kwa mwaka 2019 kati yao wanaume milioni 9.5 na wanawake milioni 22.9.

“Idadi hiyo ni sawa na asilimia 86 ya lengo la kuandikisha wapiga kura milioni 22.9. Uandikishaji wa mwaka huu umekuwa wa mafanikio makubwa sana ukilinganisha na uchaguzi wa mwaka 2014 ambapo tulikadiria kuandikisha watu milioni 18.7 na waliojitokeza kujiandikisha ni milioni 11.8 sawa na asilimia 63 ya makadirio,” alisema Waziri Jafo.

Alifafanua kuwa mafaniko hayo yametokana na hamasa kubwa iliyofanywa na viongozi wa kitaifa, Ofisi ya Rais- Tamisemi ngazi ya makao makuu ya wizara, mikoa, wilaya, halmashauri, Tarafa, Kata, Mitaa na vitongoji, wadau wa maendeleo, mchango mkubwa wa wasanii ambao umesaidiwa na ushiriki wa vyombo vya habari kuhamasisha umma.

Akizungumzia takwimu za uandikishaji wapigakura kimkoa, alisema jumla ya mikoa 26 imeshiriki katika zoezi la uandikishaji ambapo Dar es Salaam ilishika nafasi ya kwanza kuandikisha kwa asilimia 108.

Aidha, mkoa wa Pwani uliandikisha asilimia 96, Mwanza asilimia 95, Tanga asilimia 90, Singida asilimia 90, Morogoro asilimia 89, Mbeya asilimia 83, Ruvuma asilimia 88, Katavi asilimia 88, Mtwara asilimia 86, Dodoma asilimia 85, Rukwa asilimia 85 na Arusha asilimia 85.

Pia, Lindi asilimia 84, Iringa asilimia 84, Mara asilimia 80, Kilimanjaro asilimia 79, Geita asilimia 79, Manyara asilimia 78, Tabora asilimia 78, Songwe asilimia 78, Kagera asilimia 78, Shinyanga asilimia 76, Simiyu asilimia 76, Njombe asilimia 75 na Kigoma asilimia 65.

Alieleza kuwa ujumla mikoa yote na halmashauri zimefanya vizuri katika uandikishaji wa wapiga kura, kwani hakuna mkoa wala Halmashauri yoyote iliyoandikisha chini ya asilimia 50.

Alitaja mikoa iliyofanya vizuri kuwa ni pamoja na Dar es Salaam asilimia 108, Pwani uliandikisha asilimia 96, Mwanza asilimia 95, Tanga asilimia 90, Singida asilimia 90.

Aidha, alitaja halmashauri tano zilizofanya vizuri kuwa ni pamoja na Mlele DC asilimia 152, Ngorongoro DC asilimia 129, Kibiti DC asilimia 126, Temeke asilimia 122 na Monduli asilimia 122.

Jafo alisema halmashauri 5 zilizofanya vizuri kuandikisha wapiga kura wengi zaidi kuwa ni Temeke ambao wameindikisha wapigakura 879,619 (asilimia 122), Ilala iliyoandikisha wapigakura 820,600 (asilimia 111) manispaa ya Mwanza iliyoandikisha 224,901 (asilimia 105), Ubungo MC imeandikisha 542,728 (asilimia 103) na Kinondoni iliyoandikisha 569872 (asilimia 96).

Halmashauri zilizofanya vizuri ni Mlele iliyoanikisha wapigakura 27,196 (asilimia 152), Ngorongoro DC iliyoandikisha 9622 (asilimia 129), Kibiti DC iliyoandikisha 60,539kwaa asiilimia  CCmujibu wa idadi ya wapigakura

Akizungumzia changamoto za awali kabla ya kuongeza siku tatu, Jafo alisema baada ya kuanza uandikishaji Oktoba 8 mwaka huu, walibaini changamoto kadhaa.

Alitaja changamoto hizo kuwa ni pamoja na hali ya mvua katika baadhi ya maeneo, wananchi kuchanganya na zoezi la uboreshaji wa Dafari la Kudumu la wapiga kura na baadhi ya vituo kuwa mbali na kuwa ngumu kwa wananchi kufikiwa.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Kapinga: Usambazaji umeme vijijini mwisho Desemba 2023

Spread the love  NAIBU Waziri wa Nishati, Judith Kapinga, amesema ifikapo mwezi...

Habari za Siasa

Mgongano wa kimasilahi wamhamisha Chande TTCL

Spread the love  ALIYEKUWA Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO),...

Habari za SiasaTangulizi

Mgawo wa umeme: Rais Samia ampa miezi sita bosi mpya TANESCO

Spread the love  RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amempa miezi sita Mkurugenzi...

Habari za Siasa

Rais Samia avunja bodi ya REA

Spread the loveRAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amemteua Balozi Jacob Kingu, kuwa...

error: Content is protected !!