Friday , 19 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Serikali yatoa jipya wizi wa kompyuta za DPP
Habari za SiasaTangulizi

Serikali yatoa jipya wizi wa kompyuta za DPP

Dk. Augustine Mahiga, Waziri wa Katiba na Sheria (kulia) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani)
Spread the love

SERIKALI imekanusha madai ya Kompyuta za Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka Tanzania (DPP), zenye taarifa za watuhumiwa wa uhujumu uchumi, kuibiwa na watu wasiojulikana. Anaripoti Regina Mkonde … (endelea).

Dk. Augustine Mahiga, Waziri wa Katiba na Sheria, amesema kompyuta zilizoibiwa ni za Ofisi ndogo ya DPP mkoa wa Dar es Salaam na siyo Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka nchini.

“Ukweli ni kwamba, ofisi ambayo imevunjwa na vipande vya kompyuta vimechukuliwa, ni ofisi ya Mkoa wa Dar es Salaam,” ameeleza Dk. Mahiga.

Dk. Mahiga amesema Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DPP), Biswalo Mganga haijaguswa na wizi huo.

“Vyombo vya habari vimetoa taarifa, kwa mfano gazeti la leo linasema nyaraka muhimu zilizo mikononi mwa DPP zinazohusiana na wahalifu walioko mahakamani au gerezani. Kompyuta zimeibiwa. Ofisi ya mkurugenzi mkuu anayeshughulikia mashataka ya serikali haikuguswa,” amesema Dk. Mahiga.

Dk. Mahiga ameeleza kuwa, wizi huo haujaathiri zoezi la msamaha wa watuhumiwa wa uhujumu uchumi, wanaokiri makosa yao na kurejesha fedha wanazodaiwa kuiba, hivyo linaendelea kama kawaida.

“Ofisi ya DPP nyaraka alizonazo na anazofanyia kazi hazijaguswa, hivyo kitendo cha uhalifu hakijaathiri matatizo ya uhujumu uchumi,” amesema Dk. Mahiga.

Aidha, Dk. Mahiga amesema Jeshi la Polisi linafanya uchunguzi wa tukio hilo, na kuwataka wananchi kuondoa hofu.

“Na polisi wanaendelea na upelelezi wa hivyo vilivyochukuliwa. Lakini nyaraka zote zipo, taarifa zote zipo na zoezi linaendelea. Upelelezi unafanywa na Polisi,  muwache polisi washughulike nayo,” amesema Dk. Mahiga.

Hivi karibuni ziliibuka taarifa zilizodai kwamba, watu wasiojulikana wamevunja Ofisi ya DPP na kuiba kompyuta zenye taarifa muhimu za watuhumiwa wa uhujumu.

Taarifa hizo zilidai kuwa, wizi huo umefanyika kwa ajili ya kuvuruga zoezi la msamaha wa watuhumiwa, waliokiri makosa yao, na kukubali kurejesha fedha na au mali wanazodaiwa kuiba.

Zoezi hilo linatekelezwa na Ofisi ya DPP kwa kushirikiana na Mahakama. Ikiwa ni utekelezaji wa ushauri wa Rais John Magufuli alioutoa hivi karibuni, wa kusamehe watuhumiwa wa uhujumu uchumi watakaoomba msamaha na kurejesha fedha walizoihujumu serikali.

Rais Magufuli alishauri watuhumiwa hao kuomba msamaha ndani ya siku saba, ili waachwe huru na kuungana na familia zao. Watuhumiwa hao walitakiwa kuwasilisha maombi yao ya msamaha kwa DPP Mganga kuanzia tarehe 23 hadi 28 Septemba 2019.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

KimataifaTangulizi

Mkuu wa majeshi Kenya afariki, Ruto atangaza maombolezo

Spread the loveRais wa Kenya, William Ruto ametangaza maombezo ya siku tatu...

Habari za SiasaTangulizi

Tanzania, Uturuki zanuia kukuza biashara, uwekezaji

Spread the loveSERIKALI za Tanzania na Uturuki zimekubaliana kuendeleza dhamira ya kuimarisha...

Habari za Siasa

Tume huru ya uchaguzi yatangaza ajira watendaji daftari wapiga kura

Spread the love  TUME Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), imetangaza nafasi...

Habari za SiasaTangulizi

Chadema yatangaza ruti awamu ya pili maandamano

Spread the love  CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimesema awamu ya...

error: Content is protected !!