Friday , 3 May 2024
Home Kitengo Habari Kimataifa Trump aanza kuonja machungu
Kimataifa

Trump aanza kuonja machungu

Donald Trump
Spread the love

RAIS wa Marekani, Donald Trump ameanza kuonja machungu baada ya mchakato wa kung’olewa kushika kasi. Inaripoti Mitandao ya Kimataifa … (endelea).

Kupitia tamko la Nancy Pelosi, Spika wa Bunge la nchi hiyo alilolitoa tarehe 25 Septemba 2019, inaelezwa kuwa ni hatua ya awali ya mchakato huo.

Shirika la Habari la Ufarasa (AFP), inaeleza kuwa hatua ya spika huyo ni kufuatia madai ya kuwa tarehe 25 Julai 2019, Trump alizungumza kwa njia ya simu na Rais wa Ukraine, Volodymyr Zelensky kutaka msaada wa kumuangamiza mpinzani wake kwenye kampeni ijayo ya Uchaguzi Mkuu wa nchi.

Uchaguzi huo unaotarajiwa kufanyika mwaka 2020 ambapo katika mazungumzo hayo, Trump inadaiwa alimshinikiza Rais Zelensky kutafuta njia za kuchafua sifa ya makamu wa rais wa zamani, Joe Biden na mtoto wake, Hunter.

Makamu huyo wa rais ameonesha nia ya kuwania nafasi hiyo kupitia tiketi ya Chama cha Democratic, hivyo kuzidisha joto la uchaguzi huo kwa kutoa upinzani kwa Rais Trump ambaye atakuwa akitetea nafasi yake baada ya kumaliza kipindi cha kwanza cha uongozi wake.

Lakini jana Nancy alisema “inasikitisha sana kufikiria kwamba rais wetu anaweza kufanya kosa la kufunguliwa mashtaka. Ni ngumu unajua? Ni ngumu kusema tumefika katika hali hiyo,” alisisitiza Spika Pelosi akitoa taarifa hiyo kwa njia ya televisheni.

Kupitia tangazo lake Spika Nacy alisema uchunguzi maalumu utafanywa ili kubaini ukweli kisha kura zitapigwa na wabunge kupata fursa ya kuamua.

Ikiwa uchunguzi huo utaendelea, Bunge la Congress litapigia kura mashtaka yoyote yatakayobainika na kwa kuwa chama cha Democrats ndio kina wawakilishi wengi katika muhimili huo lo kinaweza kupitisha umuzi mgumu dhidi ya Rais Trump.

Hata hivyo, Trump amekanusha vikali madai hayo na kudai kuwa mazungumzo yalikuwa ya kirafiki huku akizitaja juhudi za kumtuhumu kama hila chafu dhidi yake.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaKimataifa

Mwanamke Rwanda ataka kupambana tena na Kagame

Spread the loveKIONGOZI wa kihistoria wa upinzani nchini Rwanda, Victoire Ingabire Umuhoza,...

Habari MchanganyikoKimataifa

Ruto amteua Kahariri kuwa mkuu wa majeshi

Spread the loveRAIS wa Kenya, William Ruto, amemteua Jenerali Charles Muriu Kahariri,...

Habari za SiasaKimataifaTangulizi

Tanzania, Somalia kuibua maeneo mapya ya ushirikiano

Spread the love  RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amesema Tanzania na Somalia...

KimataifaTangulizi

Mkuu wa majeshi Kenya afariki, Ruto atangaza maombolezo

Spread the loveRais wa Kenya, William Ruto ametangaza maombezo ya siku tatu...

error: Content is protected !!