July 5, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Makonda abanwa mbavu

Paul Makonda, aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam

Spread the love

PAUL Makonda, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam amebanwa mbavu, na sasa ameamua kulipiza kisasa. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea).

“Mnapiga  majungu yenu, sasa inatosha na mimi nitaanza kuwashughulikia,” ametoa kauli hiyo tarehe 25 Septemba 2019 wakati akizungumza na wakuu wa wilaya, wakurugenzi wa manispaa na watendaji wote walio chini yake.

Amesema, kila akiwapa maagizo ya kiutendaji watendaji wake, wamekuwa wakipita huku na kule na kusema hawakuelewa.

“…Mnapindua maagizo yangu na kufuata yenu, nikiuliza mnaitisha vyombo vya habari kusema mnafuata sheria. Tusishindane, tunapozidiana madaraka kila mtu atimize wajibu wake,” amesema Makonda.

Makonda aliitisha kikao hicho ili kujadili sababu za kukwama kwa miradi mbalimbali ya maendeleo. Amechukua hatua hiyo siku chache baada ya Rais John Magufuli kutoridhishwa na usimamizi wake kwa baadhi ya miradi kwenye mkoa wake.

Amelalamika kuhujumiwa na baadhi ya watendaji kwenye mkoa wake. Kutokana na hali hiyo, naye ameamua kuwachongea kwenye ngazi za juu.

Kwenye kikao hicho, Makonda amelalamikiwa kupuuzwa kwa maagizo yake huku wengine wakimpiga fita. “Haijalishi kama umenipita umri au nilikukuta serikalini lakini uko chini yangu tu.”

Amewaeleza watendaji hao kwamba, tangu awe mkuu wa mkoa hajawahi kumpiga fitna kiongozi yeyote wa idara n ahata kuandika barua kwenda juu kuhusu utendaji wake.

“Tangu nimekuwa mkuu wa mkoa huu, sijawahi kuandika barua kwa viongozi wa juu kumsema kiongozi yeyote, awe mkuu wa wilaya au wakuu wa idara. Lakini sasa nitaanza kuwasema. Nimeshamwambia Katibu Tawala wa Mkoa kila ninapotoa maagizo atoe na nakala kwenda kwa viongozi wa juu,” amesema Makonda.

Amesema, viongozi na watendaji wa mkoa huo, wanapaswa kufuata maagizo yake kwa sababu ndiye aliyepewa jukumu la kusimamia mkoa huo.

error: Content is protected !!