Monday , 6 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa JPM: Hizo ni kelele za chura, hazinizuii
Habari za Siasa

JPM: Hizo ni kelele za chura, hazinizuii

Rais John Magufuli
Spread the love

RAIS John Mgaufuli amesema, kelele zilizoibuka baada ya ndege ya Shirika la ndege la Tanzania (ATCL), kushikiliwa nchini Afrika Kusini kwa amri ya mahakama, hazikumzuia kufanya mambo yake. Anaripoti Regina Mkonde … (endelea). 

Ndege hiyo aina ya Air Bus A220-300 ilishikiliwa Afrika Kusini mwishoni mwa Agosti na kuachwa huru tarehe 4 Septemba 2019.   

Ni baada ya Mahakama Kuu ya Gauteng, nchini humo kutoa uamuzi wa kesi ya madai iliyofunguliwa na Hermanus Steyn, iliyopelekea ndege hiyo kushikiliwa.

Akizungumza katika uzinduzi wa rada jijini Dar es Salaam, leo tarehe 16 Septemba 2019 Rais Magufuli amefananisha hali hiyo, sawa na kelele za chura ambazo haziwezi kumzuia ng’ombe mwenye kiu kunywa maji.

Ameeleza, ndege hiyo ilishikiliwa kutokana na uendeshaji shughuli za ATCL kuendelea vizuri.

“Na hapa nataka niwaambie, shirika letu linaendelea vizuri sana. Ndio maana mkisikia watu wamekamata ndege zetu, msishangae sana,  hii ni kwasababu shirika letu linafanya kazi vizuri.

“Lakini kwangu mimi, hizi ni sawa na kelele za chura ambazo haziwezi kumzuia ng’ombe mwenye kiu kwenda kunywa maji,” amesema Rais Magufuli.

Wakati huo huo, amewataka Watanzania kutokubali kurudishwa nyuma katika mendeleo na baadhi ya watu.

“ ….Saa nnyingine huwa naukumbuka wimbo anaosema wao wakifunika wengine wanafunua, hawazuiliwi. Sisi hivyo hivyo, wakijaribu hivi tutafanya hivi, wakifanya hivi tunafanya hivi. Ili nchi yetu iendelee tufike tuliko panga. Watanzania tuna kiu ya maendeleo, msikubali mtu aturidishe nyuma tufike tunakotaka,” amesema Rais Magufuli.

Kuhusu uzinduzi wa rada hizo, Rais Magufuli amesema zitasaidia kuimarisha usalama wa nchi hasa wa anga pamoja na kuokoa gharama za uendeshaji wa shughuli za anga.

“Bila shaka mnafahamu nchi yetu ina mipaka ya aina tatu, ardhini, kwenye maji na angani. Na mipaka yote hii lazima tuilinde, lakini huwezi linda anga kama huna rada. Hakuna shaka kwamba,  mradi huu wa anga utaleta manufaa makubwa mbali na kuimarisha usalama wa anga zetu, mradi utaboresha usafiri wa anga,” amesema Rais Magufuli.

Mhandisi Isack  Kamwelwe, Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi amesema rada iliyozinduliwa leo katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere ni miongoni mwa rada nne zinazojengwa na serikali katika viwanja vya ndege vinne, ikiwemo Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Kilimanjaro, Mbeya na Songwe.

Eng. Kamwelwe ameeleza kuwa, usimikwaji wa rada katika Uwanja wa Ndege wa Kilimanjaro umekamilika na iko katika hatua za majaribio, wakati usimikwaji wa rada ya uwanja wa Ndege wa Mwanza uko katika hatua za kukamilisha mifumo ili majaribio yaanze.

Pia, amesema ujenzi wa jengo la kuweka mitambo ya rada katika Uwanja wa Ndege wa Songwe unaendelea na utakamilika mwanzoni mwa waka 2020, kisha rada hiyo kusimikwa.

Hamza Johari, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) amesema shughuli za ujenzi wa rada hiyo umetumia muda wa miezi 14, na kuwa gharama zilizotumika katika ununuzi wa rada hiyo pamoja na nyingine 3 umegharimu kiasi cha Sh. 67.3 bilioni.

Johari amesema kupitia mradi huo, serikali imenufaika kwa kupata vituo vidogo vya rada vya nyongeza katika viwanja vya Zanzibar na Arusha. Pia, wataalamu 53 wamepewa mafunzo kuhusu masuala ya anga nje ya nchi.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari za Siasa

Bunge laitaka Serikali kudhibiti ufisadi miradi ya mkakati

Spread the loveKAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu, imeitaka Serikali kuimarisha...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Wizara ya Uchukuzi yaomba kuongezewa bajeti na Bunge

Spread the loveWIZARA ya Uchukuzi imeliomba Bunge liidhinishe bajeti yake kwa mwaka...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Serikali kutafuta mwekezaji mwingine Bandari ya Dar es Salaam

Spread the loveSERIKALI inaendelea kutafuta mwekezaji mwingine atakayeendesha gati namba nane hadi...

Habari za SiasaTangulizi

Kinana: Hatukubali kushutumiwa kwa uongo

Spread the loveMakamu Mwenyekiti wa CCM Bara, Abdulrahman Kinana amesema viongozi wa...

error: Content is protected !!