Tuesday , 7 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Mwenge wapitisha miradi Ikungi, DC Mpogolo apongezwa
Habari za Siasa

Mwenge wapitisha miradi Ikungi, DC Mpogolo apongezwa

Spread the love

EDWARD Mpogolo, Mkuu wa Wilaya ya Ikungi, Singida amepongezwa kwa kusimamia miradi ya maendeleo ndani ya muda mfupi tangu ateuliwe kwenye nafasi hiyo. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea).

Pongezi hizo zimetolewa na Mzee Mkongea Ally, Kiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa wakati Mwenge wa Uhuru ulivyofika kukagua miradi ya maendeleo wilayani humo.

Miradi mitano ya maendeleo iliyokaguliwa na kuzinduliwa ni pamoja na vyumba viwili vya madarasa katika Shule ya Msingi Darajani, mradi wa maji uliopo Kijiji cha Ighuka, mnara wa mwenge wa kumbukumbu ya Baba wa Taifa, Mwl. Julius Nyerere na ukumbi wa Halmashauri ya Ikungi ambapo miradi yote hiyo imegharimu kiasi cha Sh. 1.162 Bil.

Akizungumza wilayani hapo, kiongozi huyo amewataka viongozi waliopewa dhamana ya kuwatumikia wananchi kufanya kazi kwa uzalendo ili kuwafanya Watanzania waendelee kuiamini serikali yao chini ya Rais John Magufuli.

“Niwapongeze sana wananchi wa Ikungi kwa namna ambavyo mmeendelea kumuamini rais wetu Dk. Magufuli, kipekee nikupongeze DC Mpogolo kwa uzalendo wako unaouonesha toka uteuliwe na Mhe Rais kuwa Mkuu wa Wilaya hii, nikuombe uendelee kuwatumikia wananchi wetu kwa kasi hii hii uliyoanza nayo.

“Niwaombe pia ndugu zangu wa Ikungi kujitokeza kwa wingi katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa na muende kuwachagua viongozi ambao ni waadilifu na wenye kuichukia rushwa,” amesema Mzee Mtongea.

DC Mpogolo ameahidi kuendelea kusimamia miradi ya serikali kwa uadilifu pamoja na kuwatumikia wananchi hao walimuamini Rais Magufuli.

“Miradi hii imegharimu fedha nyingi, upo ujenzi wa madarasa mawili ambayo yanaakisi Sera ya Elimu Bure inayosimamiwa na Rais wetu kipenzi.

“Mradi wa maji kama sehemu ya kampeni yetu ya kumtua mama ndoo kichwani, yote hiyo ni katika kuwatumikia nyinyi wananchi wetu na zaidi kutimiza ahadi ya Rais aliyoitoa kwenu mwaka 2015,” amesema.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Jacob, Malisa wapandishwa kizimbani kwa mashtaka ya uongo mitandaoni

Spread the loveMKURUGENZI wa Shirika la Haki, Godlisten Malisa na mwanachama wa...

BiasharaHabari za Siasa

Bunge laitaka Serikali kudhibiti ufisadi miradi ya mkakati

Spread the loveKAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu, imeitaka Serikali kuimarisha...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Wizara ya Uchukuzi yaomba kuongezewa bajeti na Bunge

Spread the loveWIZARA ya Uchukuzi imeliomba Bunge liidhinishe bajeti yake kwa mwaka...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Serikali kutafuta mwekezaji mwingine Bandari ya Dar es Salaam

Spread the loveSERIKALI inaendelea kutafuta mwekezaji mwingine atakayeendesha gati namba nane hadi...

error: Content is protected !!