Thursday , 2 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Ratiba mazishi ya Mhandisi Lwajabe yatolewa
Habari Mchanganyiko

Ratiba mazishi ya Mhandisi Lwajabe yatolewa

Mugisha Brassio, ndugu wa marehemu. Picha ndogo Marehemu Mhandisi Leopord Lwajabe
Spread the love

RATIBA ya mazishi ya aliyekuwa Mkurugenzi Msaidizi wa Miradi ya Umoja wa Ulaya (EU), katika Wizara ya Fedha, Mhandisi Leopord Lwajabe, imelewa na familia yake. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Akizungumza na MwanaHALISI ONLINE, Mugisha Brassio, ndugu wa marehemu amesema, kesho jioni Jumatano tarehe 31 Julai 2019, mwili wa Mhandisi Lwajabe utachukuliwa kutoka chumba cha kuhifadhia maiti cha Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) kwenda nyumbani kwake Kinyerezi,  jijini Dar es Salaam.

Mugisha amesema, mwili nyumbani kwake mpaka siku ya Alhamisi tarehe 1 Agosti 2019 ambapo mwili wa Lwajabe utafanyiwa ibada fupi ya kuagwa hapo kwake nyumbani kwake.

Baada ya ibada hiyo, mwili wa Muhandisi Lwajabe utasafirishwa kwenda kijijini kwao Ihembe katika Kata ya Ihembe, Karagwe mkoani Kagera.

kwa mujibu wa Mugisha, mwili Mhandisi Lwajabe utafanyiwa ibada ya kuagwa na kisha kusikwa siku ya Jumamosi nyumbani kwao.

“Kesho jioni maiti itachukuliwa kutoka Muhimbili, inaenda kulala nyumbani kwake Kinyerezi. Alhamisi ibada fupi itafanyika nyumbani kwake na kuaga. Baadaye unasafirishwa kwenda Karagwe, Jumamosi mwili utazikwa ” amesema Mugisha.

Mwili wa Mhandisi Lwajabe ulipatikana ukiwa umening’inizwa juu ya mti, kwenye kichaka kilichopo maeneo ya Mkuranga, mkoani Pwani.

Mwili huo ulichukuliwa na kupelekwa kuhifadhiwa katika chumba cha maiti cha Hospitali ya Mkuranga, mkoani humo.

Baada ya ndugu wa marehemu Mhandisi Lwajabe kupewa taarifa, waliuchukua mwili wa ndugu yao na kuuhifadhi Muhimbili.

Kifo cha Mhandisi Lwajabe kimeacha utata hasa baada ya mazingira ya kutoweka kwake akiwa ofisini kwake tarehe 25 Julai 2019. Mpaka sasa, hakuna taarifa iliyotolewa na jeshi la polisi kuhusu chanzo cha kifo chake.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB yang’ara maonesho OSHA

Spread the loveBenki ya NMB imebeba tuzo ya kampuni bora kwenye sekta...

Habari MchanganyikoKimataifa

Ruto amteua Kahariri kuwa mkuu wa majeshi

Spread the loveRAIS wa Kenya, William Ruto, amemteua Jenerali Charles Muriu Kahariri,...

Habari Mchanganyiko

Chongolo aonya viongozi vijiji kutouza NIDA kwa wageni

Spread the loveMKUU wa Mkoa wa Songwe, Daniel Chongolo amewaonya viongozi wa...

Habari Mchanganyiko

TUCTA, OSHA wataka kampuni za madini kuiga ubunifu wa GGML

Spread the loveSHIRIKISHO la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA) pamoja na Wakala...

error: Content is protected !!