Thursday , 2 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Serikali yawafutia kesi polisi waliodaiwa kutorosha dhahabu
Habari Mchanganyiko

Serikali yawafutia kesi polisi waliodaiwa kutorosha dhahabu

Biswalo Mganga, aliyekuwa Mkurugenzi wa Mashtaka Tanzania (DPP)
Spread the love

SERIKALI imewafutia kesi ya uhujumu uchumi namba 1 ya mwaka 2019 Askari Polisi nane, waliokuwa wanatuhumiwa kutorosha shehena ya madini ya dhahabu Jijini Mwanza. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Hayo amesema Biswalo Mganga, Mkurugenzi wa Mashtaka Tanzania (DPP) wakati akizungumza na wanahabari leo tarehe 17 Julai 2019.

DPP Mganga amesema, baada ya kuifuta kesi hiyo, mamlaka husika ziko katika utaratibu wa kuwarejesha kazini polisi hao.

Polisi hao ni pamoja na Morice Okinda, Mkuu wa Operesheni mkoani Mwanza, F 1331 PL Matete, G 5080 D/C Maingu, G 6885 D/C Alex, G 1876 D/C Japhet, G 7244 D/C Timothy na E 6948 D/C PL Kasala.

DPP Mganga ameeleza kuwa, ameamua kuwafutia mashitala polisi hao, kwa sababu ya kulinda masilahi ya taifa.

Mnamo tarehe 11 Januari mwaka huu, polisi hao pamoja na wafanyabiashara wanne, walifikishwa katika mahakama jijini Mwanza, wakikabiliwa na mashitaka matano.

Polisi hao walidaiwa kufanya makosa katika nyakati tofauti, kati ya tarehe 4 na 5 mwezi Januari 2019.

Miongoni mwa mashitaka yaliyokuwa yanawakabili ni pamoja na, uhujumu uchumi, kula njama za kupanga uhalifu na  utakatishaji fedha.

Sakata hili liliibuka mwanzoni mwa mwezi Januari mwaka huu, ambapo Rais John Magufuli aliagiza mamlaka husika kuwachukulia hatua polisi hao, ikiwemo kuwahoji kuhusu tuhuma zinazowakabili.

Awali, Polisi hao walituhumiwa kisafirisha kinyume na sheria shehena ya madini ya dhahabu pamoja na fedha kiaso cha Sh. 305 Milioni.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB yang’ara maonesho OSHA

Spread the loveBenki ya NMB imebeba tuzo ya kampuni bora kwenye sekta...

Habari MchanganyikoKimataifa

Ruto amteua Kahariri kuwa mkuu wa majeshi

Spread the loveRAIS wa Kenya, William Ruto, amemteua Jenerali Charles Muriu Kahariri,...

Habari Mchanganyiko

Chongolo aonya viongozi vijiji kutouza NIDA kwa wageni

Spread the loveMKUU wa Mkoa wa Songwe, Daniel Chongolo amewaonya viongozi wa...

Habari Mchanganyiko

TUCTA, OSHA wataka kampuni za madini kuiga ubunifu wa GGML

Spread the loveSHIRIKISHO la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA) pamoja na Wakala...

error: Content is protected !!