Saturday , 10 June 2023
Home Habari Mchanganyiko Magunia  ya mkaa, yageuka jeneza la Naomi
Habari MchanganyikoTangulizi

Magunia  ya mkaa, yageuka jeneza la Naomi

Marehemu Naomi Marijani
Spread the love

NAOMI Orest Marijani (36), mkazi wa Gezaulole, wilayani Kigamboni, jijini Dar es Salaam, aliyeripotiwa kutoweka nyumbani kwake, tokea tarehe 15 Mei mwaka huu, sasa imethibitika kuwa hayuko tena duniani. Amefariki dunia. Anaandika Faki Sosi … (endelea).

 Anayetuhumiwa kukatisha maisha ya binti huyo mrembo, ni mume wake, Khamis Said Luwongo (Meshack), kufuatia kinachoitwa, “ugomvi wa kimapenzi.”

Mkuu wa upelelezi wilaya ya Kigamboni, SP Thobias Walelo anaeleza kuwa jeshi la polisi, linamshikilia Meshack kwa tuhuma za mauaji ya mkewe, na kwamba baada ya kutekeleza unyama wake huo, aliuchukua mwili wake na kuuchoma moto ili kuficha ushahidi.”

Anasema, “mara baada ya mauaji hayo, Khamis Said Luongo, aliuchukua mwili wa Naomi na kuuweka kwenye shimo alilochimba kwenye banda la kufugia kuku. Baadaye aliweka mkaa gunia mbili na mafuta ya taa na kisha kuwasha moto uliowaka muda mrefu sana na mwili wote kuteketea kuwa majivu.”

Anaongeza, “kutokana hapo, Meshack aliupakia mwili wa marehemu Naomi kwenye gari lake na kuufikisha kwenye shamba analolimili, lililopo eneo la Vikindu, wilayani Mkuranga, mkoani Pwani. Akachimba shimo na kisha kuufikia. Juu ya eneo hilo, akapanda mgomba.”

Naomi Marijani (Sadra), mfanyabiashara na mwenyeji wa mkoa wa Kilimanjaro, ameacha mtoto mmoja, aitwaye Grecious mwenye umri wa miaka saba.

Mkuu wa Upelelelezi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Camilius Wambura, amethibitisha kutokea tukio hilo, na kwamba  tayari mtuhumiwa huyo anashikiliwa na polisi mkoa wa Temeke.

Amesema, “tumeanza kuchunguza huyu mwanamke yuko wapi? Amepoteaje? Nini kimefanyika.”

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

MichezoTangulizi

Benki ya NBC yakabidhi kombe la ubingwa wa ligi kuu kwa Yanga

Spread the loveMDHAMINI Mkuu wa ligi ya NBC, Benki ya Taifa ya...

BiasharaTangulizi

TLS wajitosa sakata la ukodishaji wa bandari

Spread the love  CHAMA cha wanasheria Tanzania (TLS), kimejitosa katika sakata la...

BiasharaTangulizi

Ngoma bado mbichi mkataba wa Bandari

Spread the love  SAKATA la mkataba wa uendeshaji, uendelezaji na uboreshaji wa...

BiasharaTangulizi

Mkurugenzi TPA: Mkataba unaweza kuvunjwa

Spread the loveMKURUGENZI Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA),...

error: Content is protected !!