Monday , 29 May 2023
Home Habari Mchanganyiko Serikali yawafutia kesi polisi waliodaiwa kutorosha dhahabu
Habari Mchanganyiko

Serikali yawafutia kesi polisi waliodaiwa kutorosha dhahabu

Biswalo Mganga, aliyekuwa Mkurugenzi wa Mashtaka Tanzania (DPP)
Spread the love

SERIKALI imewafutia kesi ya uhujumu uchumi namba 1 ya mwaka 2019 Askari Polisi nane, waliokuwa wanatuhumiwa kutorosha shehena ya madini ya dhahabu Jijini Mwanza. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Hayo amesema Biswalo Mganga, Mkurugenzi wa Mashtaka Tanzania (DPP) wakati akizungumza na wanahabari leo tarehe 17 Julai 2019.

DPP Mganga amesema, baada ya kuifuta kesi hiyo, mamlaka husika ziko katika utaratibu wa kuwarejesha kazini polisi hao.

Polisi hao ni pamoja na Morice Okinda, Mkuu wa Operesheni mkoani Mwanza, F 1331 PL Matete, G 5080 D/C Maingu, G 6885 D/C Alex, G 1876 D/C Japhet, G 7244 D/C Timothy na E 6948 D/C PL Kasala.

DPP Mganga ameeleza kuwa, ameamua kuwafutia mashitala polisi hao, kwa sababu ya kulinda masilahi ya taifa.

Mnamo tarehe 11 Januari mwaka huu, polisi hao pamoja na wafanyabiashara wanne, walifikishwa katika mahakama jijini Mwanza, wakikabiliwa na mashitaka matano.

Polisi hao walidaiwa kufanya makosa katika nyakati tofauti, kati ya tarehe 4 na 5 mwezi Januari 2019.

Miongoni mwa mashitaka yaliyokuwa yanawakabili ni pamoja na, uhujumu uchumi, kula njama za kupanga uhalifu na  utakatishaji fedha.

Sakata hili liliibuka mwanzoni mwa mwezi Januari mwaka huu, ambapo Rais John Magufuli aliagiza mamlaka husika kuwachukulia hatua polisi hao, ikiwemo kuwahoji kuhusu tuhuma zinazowakabili.

Awali, Polisi hao walituhumiwa kisafirisha kinyume na sheria shehena ya madini ya dhahabu pamoja na fedha kiaso cha Sh. 305 Milioni.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Kirigini kuzikwa leo Butiama

Spread the love  MWILI wa aliyekuwa Mbunge wa Musoma Vijijini (1980-1985), Herman...

Habari MchanganyikoTangulizi

Jeshi la Polisi kushirikiana na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam katika utafiti

Spread the love  JESHI la Polisi Nchini limesema kuwa katika kukabiliana na...

Habari Mchanganyiko

Kampeni ya Samia Legal Aid yazinduliwa Manyara, kesi 45 zapokelewa

Spread the love  KAMPENI ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia, imezinduliwa...

Habari Mchanganyiko

NMB ya kwanza kuzindua Malipo kwa QR na UnionPay International

Spread the loveBENKI ya NMB kwa kushirikiana na UnionPay International (UPI), wamezindua...

error: Content is protected !!