Friday , 3 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Nyalandu aonja machungu ya kuwa upinzani
Habari za Siasa

Nyalandu aonja machungu ya kuwa upinzani

Spread the love

LAZARO Nyalandu, aliyewahi kuwa Mbunga wa Singida Kaskazini kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), ameeleza kufedheheshwa na kadhia ya kwenda kuripoti Kituo cha Polisi cha kati mkoani Singida mara kwa mara kama alivyotakiwa. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea).

Leo tarehe 31 Mei 2019 amesema, kadhia hiyo inarudisha nyuma ufanisi wa utendaji kazi kwenye chama hicho ili kufikia leo walilojiwekea la ‘Chadema ni Ushindi’.

Akizungumza na wanahabari baada ya kuripoti kituoni hao na kuambiwa kwamba, OCD hayupo na kutakiwa kurejea tarehe 4 Julai 2019 amesema, hatua ya kuripoti kituoni hapo mara kwa mara inaminya muda wa kuifanya kampeni hiyo kufanikiwa.

Nyalandu ambaye aliwahi kuwa Waziri wa Maliasili na Utalii katika Awamu ya Nne chini ya Rais Jakaya Kikwete na wenzake wawili, walikamatwa kwa tuhuma za kufanya kikao cha ndani bila kibali pia tuhuma za kujihusisha na vitendo vya rushwa.

Nyalandu aliyejiunga na Chadema mwaka 2017 amesema kuwa, nchi hii inaendeshwa kwa mujibu wa sheria hivyo hawana budi kutekeleza wito wa Jeshi la Polisi mkoani humo lililowataka kuripoti kituoni hapo.

“Njoo leo mara njoo kesho, hii ina madhara makubwa” amesema Nyalandu na kuongeza “naomba tusikate tamaa kwa haya yanayoendelea sasa, tuendelee kupambana. Tutaendelea na mikutano yetu ya ndani katika kata zote 16.”

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Chadema waendelea kulilia katiba mpya

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeendelea kudai upatikanaji wa...

Habari za SiasaTangulizi

Chadema kumshtaki Rais Samia

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimetishia kumfungulia kesi ya...

Habari za Siasa

Tume huru ya uchaguzi yatangaza uchaguzi mdogo Jimbo la Kwahani

Spread the love  TUME Huru ya Taifa ya Uchaguzi, imetangaza uchaguzi mdogo...

AfyaHabari za Siasa

Dk. Biteko aagiza utoaji huduma saratani usiwe wa kibaguzi

Spread the loveNaibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko...

error: Content is protected !!