Wednesday , 27 September 2023
Home Kitengo Maisha Afya Misoprostol yatumika kutoa mimba, serikali yatoa agizo
AfyaHabari Mchanganyiko

Misoprostol yatumika kutoa mimba, serikali yatoa agizo

Spread the love

SAKATA la watoto wa kike na kina mama kutumia vibaya dawa aina ya Misoprostol kwa ajili ya kutoa mimba, limeibuka bungeni ambapo serikali imetoa agizo jipya kwa maduka ya dawa za binadamu (Famasi) nchini. Anaripoti Regina Mkonde…(endelea).

Akizungumza leo tarehe 31 Mei 2019 bungeni Jijini Dodoma kwa niaba ya Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Stansilaus Nyongo, Naibu Waziri wa Madini, amepiga marufuku  famasi kuuza dawa hizo kwa wateja wasiokuwa na cheti cha daktari.

Nyongo amesema kabla ya famasi hizo kumuuzia dawa mteja, lazima wahakikishe mteja husika na cheti cha daktari kinachothibisha kwamba ana tatizo ambalo linatibiwa na dawa hizo.

“Dawa hizi zinatakiwa zitolewe chini ya usimamizi wa daktari, yaani daktari anatakiwa aandike dawa hiyo na mgonjwa akienda famasi aende na cheti cha kuweza kupewa dawa hizo. Kweli hizi dawa zina matumizi mengine,”  amesema Nyongo na kuongeza.

“Lakini zinaanza kuzunguka, ziko kwenye famasi na ni za kazi maalum kuzuia damu zisitoke, lakini wana zitumia vibaya sababu ‘side effect’ yake ni kutoa mimba.  Tuna washauri watu wote wenye famasi wasitoe dawa hizi bila cheti,  lazima dawa hizi daktari athibitishe aandike cheti na mgonjwa huyo apewe dawa hizo.”

Nyongo ametoa agizo hilo baada ya Mbunge Amina Mwakilagi kueleza kwamba, kumekuwepo na wimbi kubwa la kina mama na watoto wa kike kutumia vibaya dawa hizo kwa kutoa mimba zisizotarajiwa, kitendo kinachohatarisha usalama wao.

Mwakilagi amesema dawa hizo ambazo ni maalum kwa ajili ya kuzuia damu kutoka, zikitumiwa vibaya zinaweza zikasababisha athari kwa afya za wahusika, na kuhoji mkakati wa serikali katika kuhakikisha kwamba hazitumiwi vibaya.

“Kuna dawa zinaitwa Misoprostol vijana wanafundishana siku hizi wanatumia kutoa mimba , serikali ina mpango gani wa kuzuia dawa hizi,” amehoji Mwakilagi.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Kapinga: Usambazaji umeme vijijini mwisho Desemba 2023

Spread the love  NAIBU Waziri wa Nishati, Judith Kapinga, amesema ifikapo mwezi...

Habari Mchanganyiko

Wizara ya madini kurusha ndege ya utafiti wa madini Geita

Spread the loveKutokana na mchango wa wachimbaji wadogo wa madini kwenye pato...

Habari Mchanganyiko

Jafo aagiza kampuni za madini kuzingatia utunzaji mazingira, azitaka zijifunze kwa GGML

Spread the loveWAZIRI wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na...

Habari Mchanganyiko

Rais Samia apewa tano ujenzi barabara Mtwara

Spread the loveWANANCHI wa Mkoa wa Mtwara, wameishukuru Serikali ya Rais Dk....

error: Content is protected !!