Tuesday , 7 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Vituko Bunge la Spika Ndugai
Habari za SiasaTangulizi

Vituko Bunge la Spika Ndugai

Job Ndugai, aliyekuwa Spika wa Bunge Tanzania
Spread the love

STAILI ya kutishia kuvua nguo iwapo jambo fulani lisipotendwa ama kuthibiti, imeanza kupata umaarufu ndani ya Bunge la Jamhuri. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma…(endelea).

Kwa mara nyingine tena, Richard Mbogo, Mbunge wa Nsimbo (CCM) ametishia kuvua nguo wakati wa mjadala wa Wizara ya Maji tarehe 3 Mei 2019.

Ametishia hatua hiyo kwa madai kwamba, itamlazimu kufanya hivyo ikiwa ndio njia ya kupatikana maji safi na salama katika jimbo lake la Nsimbo.

Kama ya namna hiyo imetolewa hivi karibuni na Kangi Lugola, Waziri wa Mambo ya Ndani alipomtuhumu Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Prof. Mussa Assad kwamba ni muongo.

Waziri Lugola aliliambia Bunge kuwa, endapo ripoti ya CAG itakuwa ni kweli, yupo tayari kuvua nguo ikibainika kuwa taarifa zake za ukaguzi kuhusu sare hewa za Jeshi la Polisi zilizogharimu Sh. 16 Bil ni za kweli.

“Sijawahi kuona mtu muongo kama CAG, Jeshi la Polisi hakuna sare hewa. Ninaomba Maafisa wa Ofisi ya CAG twende nao stoo wakaone sare mpya za Jeshi la Polisi. Kama nasema uongo, nitavua nguo na ninaweka uwaziri wangu rehani.”

Akichangia mjadala wa bajeti ya Wizara ya Maji kwa Mwaka wa Fedha 2019/20, Mbogo alitoa vitisho hivyo kwa kuwa, suala la maji halina mbadala kwenye jimbo lake na kuitaka serikali kutatua tatizo hilo.

“Mheshimiwa mwenyekiti, suala la maji safi na salama si la mzaha, ikibidi niko tayari kuvua nguo hapa bungeni ili nipate suluhisho la upatikanaji wa maji Nsimbo.

“Kama kuonyesha niko ‘serious’ kwa jambo hili, niko tayari kufanya lolote, kama kuna jambo mnaweza kufanya mtuambie tufanye,” amesema Mbogo.

Mbogo anaungana na Dk. Mery Nagu, Mbunge wa Hanang kwamba, mzigo wa kuchangia mfuko wa maji urejeshwe moja kwa moja kwa wananchi kupitia ununuzi wa petroli na dizeli.

“Tozo hii ya Sh. 50 ni muhimu sana,” amesema Mbogo akishinikiza Bunge likubali kupitisha ongezeko la bei ya petroli na dizeli kwa wananchi.  

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Rais Samia ni Mzanzibari: Shida Iko Wapi?

Spread the loveTAIFA linakabiliwa na upungufu wa fikra sahihi. Upungufu huu unaonekana...

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Mpina mwiba CCM, ahofia kuzibwa mdomo

Spread the loveWAKATI Chama cha Mapinduzi (CCM), kikijinasibu kuwa kinara wa demokrasia...

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Mabeyo ametuepusha

Spread the loveNIMEGUSWA na uadilifu, utiifu na uaminifu wa Mkuu mstaafu wa...

Habari za SiasaTangulizi

CCM yaitaka TAKUKURU kuichunguza Chadema tuhuma alizoibua Lissu

Spread the loveCHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimeitaka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana...

error: Content is protected !!