November 27, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Msukuma: Nagu umetumwa?

Spread the love

PENDEKEZO la wabunge kutaka kuwabebesha mzigo wananchi kwa kuongeza Sh. 50 kwa kila lita ya mafuta ya petroli na dizeli, limesababisha wabunge wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kushutumiana. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).    

Pendekezo hilo linalenga kutanua mfuko wa maji limewaingiza kwenye ‘vita’ Dk. Mary Nagu, Mbunge wa Hanang (CCM) ambaye anapendekeza mzigo huo atwishwe mwananchi huku Joseph Kisheku (Musukuma), Mbunge wa Geita (CCM) akipinga.

Dk. Nagu akichangia makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara ya Maji kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 tarehe 3 Mei 2019, aliwataka wabunge kukubali azimio la kuongeza kiasi hicho cha fedha ambazo zitatoka kwa wananchi wanunuapo dizeli na petroli.

Maelezo ya Dk. Nagu yalimtibua Msukuma ambapo aliomba taarifa kwa Job Ndugai, Spika wa Bunge, hata hivyo hakuruhusiwa.

Baada ya kuona haruhusiwi, Msukuma alisimama na kusema “mama nakuheshimu sana aisee!” kauli hiyo ilimfanya Dk. Nagu kumsikiliza na kumpa nafasi Msukuma aendelee.

Ndipo Musukuma alipomtaka Dk. Nagu alithibitishie Bunge kama ametumwa na wafanyabiashara wa petroli, na kama hakutumwa, basi afute kauli yake.

Pamoja kauli ya Msukuma, Dk. Nagu aliendelea kusimamia msimamo wake kwamba, mzigo huo uelekezwe kwa wananchi huku akimtaka Msukuma kuvumiliana.

“Musukuma asikubali wenye petroli wamtumie huku ndani kuwa hiyo pesa (Sh. 50) isitokane na petroli,” amesema Dk. Nagu.

Katika maelezo yake ya awali, Dk. Nagu alisema, mfuko wa maji umefanikisha miradi mingi na kwamba, kuimarika kwa mfuko huo kutachochea miradi mingine.

Amesisitiza kwamba, kama Bunge litarudi nyuma, juhudi za maji zitarudi nyuma huku akitaka vyanzo vingine vitafute kwa ajili ya miradi ya maji.

Kurushiana maneno kwa wabunge hao kulitokana na Musukuma kutaka wabunge kutokubali kuongeza kiasi hicho cha fedha katika mafuta kwani kufanya hivyo ni kuwabebesha wananchi mzigo.

Amesema kuondokana na tatizo la maji matatizo katika sekta nyingine pia yataondoka.

error: Content is protected !!