Monday , 6 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Rais TLS: Lissu ahojiwe
Habari za SiasaTangulizi

Rais TLS: Lissu ahojiwe

Spread the love

RAIS wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS), Dk. Rugemaliza Nshala amesema, ipo haja kwa Tundu Lissu kuhojiwa kutokana na shambulio lake. Anaripoti Faki Sosi…(endelea).

Amesema, Watanzania wanahitaji kujua ukweli kuhusu tukio hilo, serikali inapaswa kutafuta majibu ikiwa ni pamoja na kupata ukweli wa mazingira kutoka kwa Lissu ambaye kwa sasa yupo nje ya nchi kwa matibabu.

Lissu, Mbunge wa Singida Mashariki ambaye pia ni Rais Mstaafu wa TLS, alishambuliwa nyumbani kwake jijini Dodoma mchana wa tarehe 7 Septemba 2017 na watu ambao mpaka sasa hawajajulikana. Baadaye alipelekwa Kenya kwa matibabu na kisha Uholanzi ambayo bado yupo huku mpaka sasa.

Akizungumzia na MwanaHALISI ONlLINE kuhusu umhimu wa serikali kusimamia uchunguzi na kutoa majibu Dk. Inshala amesema, Watanzani wana haki ya kujua tukio lililomkuta Mtanzania mwenzo kama ilivyo kwa Watanzania wote.

“Tukio hili linaaibisha nchi hasa ukimya huu ukiendelea. Hili ni suala la kitaifa. Wananchi tunahitaji kupata uhakika wa haki yetu ambayo ni haki ya kuishi iliyoelezwa kwenye Katiba yetu ibara ya 14 inayosema kuwa, kila mtu anahaki ya kuishi na kupata hifadhi,” amesema.

Rais huyo wa TLS aliyeanza kazi Jumamosi wiki iliyopita baada ya kuchaguliwa, amesisitiza kufanywa uchunguzi huo haraka ili vyombo vyenye mamlaka vijiondoe kwenye lawama.

“Mwenzetu anavyojeruhiwa, anavyopigwa risasi wewe ukikataa kuchunguza, ni kwamba yule mtu unamgeuza kuwa sio mtu wa jamii yako.

“Unakuwa tayari unambagua, ni vema mtu huyu akawa anajilinda yeye mwenyewe maana nanaona katengwa,” amesema Dk. Inshala na kuongeza;

“Tundu Lissu amepigwa risasi, tukaambiwa upelelezi tufanyika. Baadaye limekuwa suala la kejeli au kukomoana, jambo hili linaaibisha nchi yetu.”

Yeye pamoja na wanachama wa TLS amesema, bado wanaguswa na tukio hilo hasa kwa kuwa, kinaaibisha nchi.

“Hatuwezi kuendesha nchi kwa kumkomoa, mtu mambo haya yanaumiza na sio Lissu pekee, wapo watu wamepotea na hatusikii uchunguzi wowote,” anasema Dk. Nshala.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari za Siasa

Bunge laitaka Serikali kudhibiti ufisadi miradi ya mkakati

Spread the loveKAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu, imeitaka Serikali kuimarisha...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Wizara ya Uchukuzi yaomba kuongezewa bajeti na Bunge

Spread the loveWIZARA ya Uchukuzi imeliomba Bunge liidhinishe bajeti yake kwa mwaka...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Serikali kutafuta mwekezaji mwingine Bandari ya Dar es Salaam

Spread the loveSERIKALI inaendelea kutafuta mwekezaji mwingine atakayeendesha gati namba nane hadi...

Habari za SiasaTangulizi

Kinana: Hatukubali kushutumiwa kwa uongo

Spread the loveMakamu Mwenyekiti wa CCM Bara, Abdulrahman Kinana amesema viongozi wa...

error: Content is protected !!