Friday , 3 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Prof. Shivji: Kuna sheria mbovu zinatungwa
Habari za Siasa

Prof. Shivji: Kuna sheria mbovu zinatungwa

Profesa Issa Shivji
Spread the love

MSOMI wa masuala ya sheria na utawala nchini Profesa Issa Shivji, ameeleza kukerwa na mwelekeo wa utungaji sheria mbovu kwa maslahi ya wachache. Anaripoti Faki Sosi … (endelea).

Miongoni mwa mifano ya sheria mbovu alizotaja ni pamoja na Sheria ya Takwimu ya  mwaka 2018, inayomtaka mtu yoyote kutochapisha au kusambaza taarifa au chochote kuhusu takwimu mpaka apate kibali kutoka Ofisi ya  Taifa ya Takwimu (NBS).

Akizungumza katika kumbukizi ya miaka 16 ya kifo cha Jaji Francis Nyalali ilioandaliwa na taasisi ya Center for Strategic Litigation jijini Dar es Salaam leo tarehe 3 Aprili 2019 amesema, baadhi ya sheria zinatungwa kulenga watu ama kundi fulani.

“Hivi karibuni tumepitisha sheria nyingi mbovu, mfano hii Sheria ya Takwimu ambapo huwezi kufanya uchambuzi wowote wa kitakwimu na kuutoa mpaka upate kibali,” amesema.

Akimzungumzia Jaji Nyalali, Prof. Shivji amesema maisha yake yaenziwe kwa kuheshimu utawala wa sheria na kwamba, mchango wake (Jaji Nyalali) ulikuwa kwenye utawala wa sheria hivyo amelitaka taifa kusimama na urithi huo.

Jaji John Mroso amemuelezea Jaji Nyalali kwamba alikuwa anaumizwa anaposikia mahakama ikikosolewa, hasa kwenye  eneo la ucheleweshaji wa kesi.

“Wanasiasa walikuwa wakikosoa suala hilo ambapo ilimuumiza ikapelekea kusafiri kwenda nchini Marekani kwa ajili ya kupata uzoefu wa namna wanaendeshaje kesi,” amesema Jaji Mroso.

Jaji Mroso amesema, Jaji Nyalali ndiye aliyeanzisha mfumo wa kusimamia kesi za masikini bure. “Hakupendezwa na mtu yoyote aliyetaka kuingilia uhuru wa mahakama.”

Jaji Nyalali alihuduma kama Jaji Mkuu wa Tanzania kuanzia Mwaka 1977 hadi 2000 na kufariki terehe 2 Aprili 2003.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Sabaya afutiwa kesi, ruksa kugombea uongozi

Spread the loveMwendesha Mashtaka Mkuu wa Serikali DPP leo Ijumaa amefuta rufaa...

Habari za Siasa

Serikali yasaka bilioni 3 kujenga daraja Mto Mpiji

Spread the loveSerikali imesema inaendelea na juhudi za kutafuta fedha kiasi cha...

Habari za SiasaTangulizi

Chadema kwafukuta kisa chaguzi, Lissu aibua tuhuma nzito

Spread the loveCHAGUZI za kusaka viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Chadema waendelea kulilia katiba mpya

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeendelea kudai upatikanaji wa...

error: Content is protected !!