Monday , 5 June 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Zitto, Maalim Seif kuweka historia Tanga
Habari za SiasaTangulizi

Zitto, Maalim Seif kuweka historia Tanga

Spread the love

MAALIM Seif Shariff Hamad, aliyekuwa Makamu wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na Zitto Kabwe, Kiongozi Mkuu wa Chama cha ACT-Wazalendo leo tarehe 4 Aprili 2019 wanatarajiwa kufanya makubwa mkoani Tanga. Anaripoti Regina Mkonde … (endelea).

Jumla ya madiwani 10, wenyeviti wa serikali za mitaa 62, wanachama wapya 7,641 wanatawajiwa kupokewa na chama hicho huku matawi mapya 81 yakifunguliwa kwenye ziara inayoanza leo mkoani humo.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo iliyotolewa na mratibu wa ziara ya viongozi wa ACT-Wazalendo mkoani Tanga, Mbarala Maharagande, Zitto pamoja na Maalim Seif wanaanza ziara ya siku mbili ya ujenzi wa chama hicho.

“Shughuli zitakazofanyika ni pamoja na kusimamia upatikanaji wa viongozi wa chama kwa maana ya uchaguzi wa ndani ya chama, kukagua na kuzindua matawi mapya 81.

“Kutoa kadi kwa wanachama wapya na awali 7,641 kwa awamu ya kwanza, pia kuwapokea madiwani 10 na wenyeviti wa serikali za mtaa 62 waliohama,” inaeleza sehemu ya taarifa hiyo.

Hayo yanafanyika baada ACT-Wazalendo kutikisa visiwani Zanzibar ambapo kambi ya Chama cha Wananchi (CUF) imevurugwa baada ya waliokuwa wanachama wake kumfuata Maalim Seif ACT-Wazalendo.

Shughuli zingine zitakazofanyika katika ziara hiyo inayoanza Tanga Mjini leo na kumalizikia wilayani Pangani kesho tarehe 5 Aprili 2019, ni kuhakikisha chama hicho kinatengeneza uongozi imara wa mkoa, wilaya na kata kuelekea Uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaotarajiwa kufanyika Novemba 2019.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

MichezoTangulizi

Yanga malizeni ugomvi na Fei Toto – Rais Samia

Spread the love  RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Samia...

Habari MchanganyikoTangulizi

Kifo cha mwanafunzi UDOM: Tume yamsafisha naibu waziri

Spread the loveTUME ya Haki za Binadamu na Utawala Bora nchini (THBUB),...

Habari MchanganyikoTangulizi

Bosi NIC apandishwa kizimbani, akabiliwa na mashitaka 365

Spread the love  ALIYEKUWA Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Bima la Taifa...

Habari za Siasa

Lusinde: CCM hatuliachii ng’o jimbo la Moshi Mjini

Spread the loveMJUMBE wa Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi (NEC), Livingston...

error: Content is protected !!