Sunday , 28 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Wabunge wa ‘Maalim Seif’ wategwa CUF
Habari za Siasa

Wabunge wa ‘Maalim Seif’ wategwa CUF

Spread the love

UONGOZI wa Chama cha Wananchi (CUF) umeanza kushinikiza wabunge waliokuwa wakimuunga aliyekuwa Katibu Mkuu wa chama hicho, Maalim Seif Shariff Hamad kwenda kuungama. Anaripoti Regina Mkonde … (endelea).

Kauli ya kuwataka wabunge hao kuomba radhi uongozi wa chama hicho kwa madai ya kutukanwa na wabunge waliokuwa nyuma ya Maalim Seif imetolewa leo tarehe 26 Machi 2019 na Halifa Suleiman Halifa, Katibu Mkuu wa chama hicho.

Amesema, wabunge hao wanapaswa kufanya hivyo kabla hatua zingine hazijachukuliwa na uongozi wa CUF na kuwa, wakikaidi mwenyekiti wa chama hicho Taifa, Prof. Ibrahim Lipumba atawachukulia hatua.

“Wabunge wajue kuwa waliingia katika bunge kwa tiketi ya CUF, wasije wakadhania kuwa aliowapeleka bungeni ni Maalim Seif (Maalim Seif Shariff Hamad), wametutukana sana, wametuhujumu sana lakini mwenyekiti alisema tunanyoosha mkono wa msamaha kwao

“Yote yaliyopita yamepita sasa, tunataka kitu kimoja mashirikiano yao, wala hatupati tabu kuwaandikia barua tuwaite. Waje ofisini kwa mwenyekiti wa chama wapeane mikono, waje wamuone katibu mkuu, wasipofanya hivyo sijui mwenyekiti atafanya nini baadaye,” amesema Halifa Kauli hiyo imetolewa leo katika Ofisi Kuu ya chama hicho Buguruni jijini Dar es Salaam.

Pia Halifa amesema, rasilimali za CUF zitatumika kuimarisha chama hicho na si vinginevyo, hivyo ametoa wito wabunge hao kutotumia rasilimali hizo kuimarisha chama kingine.

Amesema, chama chake hakitakubali kuona rasilimali hizo zinatumika kwa ajili ya kuimarisha Chama cha ACT-Wazalendo ambacho hivi karibuni kimempokea Maalim Seif, aliyekuwa Katibu Mkuu wa CUF.

“ Sisi hatutakubali kuona wanatumia pesa na rasimiali za CUF kuiimarisha ACT, kuna mawili, wajiandae kurudi au  wasubiri mengine.

“Hatuwezi kusubiri wao wajiimarishe kwenye majimbo bila ya kushirikiana na chama ili baadaye waje wagombee kupitia ACT-Wazalendo,” amesema Halifa.

Aidha, Halifa amewakumbusha wabunge hao kuwa, waliingia bungeni kwa tiketi ya CUF hivyo wanapaswa kushirikiana nacho katika utekelezaji wa shughuli zao majimboni na kwamba, wakienda kinyume na hapo Prof. Lipumba atawachukulia hatua.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mavunde aibana kampuni kutimiza masharti ya mkataba

Spread the loveWaziri wa Madini, Anthony Mavunde ameitaka Kampuni ya Xin Tai...

Habari za Siasa

Sauti ya Watanzania waeleza sababu za kuiunga mkono Chadema

Spread the love  KIKUNDI kinachojipambanua katika kupigania rasilimali na uhuru wa nchi,...

Habari za SiasaKimataifaTangulizi

Tanzania, Somalia kuibua maeneo mapya ya ushirikiano

Spread the love  RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amesema Tanzania na Somalia...

Habari za Siasa

ACT: Waongoza watalii wapate maslahi yao inavyostahili

Spread the loveCHAMA cha ACT-Wazalendo kimeitaka serikali kuhakikisha inasimamia maslahi stahiki ya...

error: Content is protected !!