Monday , 6 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Simu ya Prof. Lipumba ‘yakimbiza polisi’ 
Habari za SiasaTangulizi

Simu ya Prof. Lipumba ‘yakimbiza polisi’ 

Spread the love

SIMU iliyopigwa na Prof. Ibrahim Lipumba, Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF) anayetambuliwa na Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, ‘iliwapoza’ Jeshi la Polisi lililofika kuzuia mkutano huo leo tarehe 12 Machi 2019 na hatimaye kuondoka. Anaripoti Regina Mkonde … (endelea).

Jeshi la Polisi Kanda ya Ilala likiongozwa na Kamanda, Zuberi Chembera lilifika Ofisi Kuu ya CUF Buguruni jijini Dar es Salaam kuzuia mkutano huo kutokana na kuwepo kwa zuio la mahakama.

Baada ya kuwepo kwa vuta nikuvute kati ya jeshi hilo na baadhi ya viongozi wa CUF, Prof. Lipumba alitoa simu na kupiga mahali mazungumzo ambayo yalidumu kwa muda mchache.

Baada ya simu hiyo, msimamo wa polisi ulibadilika ambapo magari yaliyokua yamebeba polisi pamoja na moja la maji ya washawasha yaliondoka eneo la tukio huku mkutano ukiendelea.

Hata Prof. Lipumba alipoulizwa alikuwa akiongea na nani, alijibu “nilikuwa naongea na jamaa zangu, mimi ni mtu mzito siwezi kukwambia.”

Awali; Jeshi hilo lilifika katika ukumbi wa mkutano ofisini hapo Buguruni jijini Dar es Salaam na kuamuru kikao hicho kisitishwe kwa kuwa, kuna zuio la mahakama.

Hata hivyo, wajumbe wa mkutano huo walianza kuweka mgoma kutii agizo hilo kwa madai kwamba, hakuna taarifa yoyote ya maandishi iliyofikishwa kwao ikielekeza kuzuia mkutano huo.

Wajumbe wa mkutano huo kutoka maeneo malimbali nchini walifika kwenye ofisi hiyo kuhudhuria Mkutano Mkuu uliopangwa kuanza leo tarehe 12-15 Machi 2019 pamoja na malengo mengine pia kuchagua viongozi wapya.

Kwenye mkutano huo, Sisty Nyahoza, Naibu Msajili aliwaambia wajumbe wa mkutano huo kwamba, unafanyika kwa mujibu wa Katiba ya CUF na kwamba, ndio maana amefika kuwakilisha Ofisi ya Msajili.

Kwenye mkutano huo Nyahoza amewapongeza CUF Lipumba kwa kufanikiwa kusajili Bodi ya Wadhamini pamoja na kuhimili mikiki ya mahakama kwa dhamira ya kulinda chama hicho.

Kufika kwa Jeshi la Polisi kwenye viwanja vya mkutano huo kulibadili taswira ya eneo hilo huku wajumbe wakionekana kukasirishwa na dalili za kutaka kuvuruga mkutano huo.

Prof. Lipumba na wanaomtii walipanga kufanya mkutano huo kwa siku nne mfululizo. Hata hivyo, baada ya wajumbe kuwasili leo asubuhi kwenye Ukumbi wa Mkutano, zoezi la usajili na uhakiki lilianza kutekelezwa.

Wakati zoezi la uhakiki wa wajumbe wa mkutano huo likiendelea, ghafla polisi walifika eneo la mkutano huo na kufanya mazungumzo na baadhi ya viongozi wa CUF.

Hata hivyo, polisi walimtaka Prof. Lipumba kuvunja mkutano huo kwa kuwa, kuna zuio la mahakama. Polisi walianza kuzungumza na viongozi wengine wa chama hicho ikiwa ni pamoja na Magdalena Sakaya, Naibu Katibu Mkuu, Magdalena Sakaya na Abdul Kambaya, Mkurugenzi wa Habari na Mawasiliano ya Umma.

Pamoja na taarifa hiyo viongozi hao waliendelea kusema kuwa, watafanya mkutano huo kwa kuwa hawajapokea nakala yoyote inayozuia mkutano huo.

Wakati majadiliano hayo yakiendelea, polisi walikuwa na difenda mbili zikiwa na askari polisi na gari moja ya maji ya kuwasha yalikuwa yameegesha nje ya maeneo hayo.

Kelele za chini kwa chini zilianza kusikika “hata kama umekuja na zuio la mahakama sisi hatulipokei kwa sababu wewe huna mamlaka ya kulileta na hapa hatuondoki mkitaka mtuue wote.”

Ndipo Prof. Lipumba alitoka na kuanza kufanya mazungumzo na polisi na baadaye kupiga simu ambapo ilisababisha keshi hilo kuondoka na kuacha mkutano ukiendelea.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari za Siasa

Bunge laitaka Serikali kudhibiti ufisadi miradi ya mkakati

Spread the loveKAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu, imeitaka Serikali kuimarisha...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Wizara ya Uchukuzi yaomba kuongezewa bajeti na Bunge

Spread the loveWIZARA ya Uchukuzi imeliomba Bunge liidhinishe bajeti yake kwa mwaka...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Serikali kutafuta mwekezaji mwingine Bandari ya Dar es Salaam

Spread the loveSERIKALI inaendelea kutafuta mwekezaji mwingine atakayeendesha gati namba nane hadi...

Habari za SiasaTangulizi

Kinana: Hatukubali kushutumiwa kwa uongo

Spread the loveMakamu Mwenyekiti wa CCM Bara, Abdulrahman Kinana amesema viongozi wa...

error: Content is protected !!