April 11, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Mama aliyejifungua watoto wanne apiga yowe

Spread the love

RADHIA Solomon (24), mzazi aliyejifungua watoto wanne kwa pamoja (mapacha) yupo kwenye wakati mgumu wa kukabili changamoto ya kumudu malezi ya watoto hao. Anaripoti Faki Sosi… (endelea).

Radhia ameieleza MwanaHALISI ONLINE kuwa, hali hiyo inatokana na ukata wa kifedha kwake na mzazi mwenzake.

Amesema “watoto hawa wanatumia maziwa ya kopo ambapo wanatumia kopo moja kwa wiki. Kopo hilo linagharimu shilingi elfu 40  ambapo  sisi tunashindwa kumudu.”

Ameomba kwa watu wataokaoguswa, wamsaidie taulo za watoto, maziwa na huduma za afya  sambasamba na mazingira anayoyatumia kuwalea watoto hawa.

Amesema, licha kuwa serikali kuweka utaratibu kwa mzizi atakayejifungua watoto zaidi ya wawili atasaidiwa na kwenye malezi lakini yeye ni mwezi wa pili hajapata msaada ingawa alifika Ustawi wa Jamii Wilaya ya Kinondoni kujieleza.

Kwa yoyote atakayeguswa na hili awasiliane na Radhia kwa namba 0682 604 202.

Tazama video hapo chini kujua alichosema Mama huyo.

error: Content is protected !!