Friday , 19 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Waziri Mkuu awachimba mkwara mawaziri wake
Habari za Siasa

Waziri Mkuu awachimba mkwara mawaziri wake

Spread the love

WAZIRI Mkuu Kassm Majaliwa amewataka mawaziri wote kuhakikisha wanahudhuria katika vikao vya kamati za kudumu za bunge. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma … (endelea).

Majaliwa alitoa wito huo jana muda mfupi kabla ya kumkaribisha Waziri wa Fedha na Mipango Dk. Philip Mpango, kuwasilisha maelezo ya Wizra hiyo kuhusu Mapendekezo ya serikali ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa na ya kiwango na ukomo wa Bajeti ya serikali kwa mwaka 2019/20 Jijini hapa.

Alisema kuwa baada ya kupokea mapendekezo hayo ni wajibu wa wabunge sasa kuhakikisha wanayasoma mapendekezo ili kuona ni wapi ambapo panafaa kuboreshwa zaidi.

Alisema baada ya kumaliza ziara kamati zitakaa na kuanza kujadili mpango uliowasilishwa hivyo ni wajibu wa kila mawaziri wote kufika kwenye vikao vya kamati kwa lengo la kutoa ushirikiano na kusikiliza mapendekezo ya kamati husika.

“Serikali kuu ilisha toa maagizo thabiti kwa mawaziri wote kuhakikisha wanahudhuria vikao vya kamati kadri kamati inavyowahitaji.

“Tunaamini mawaziri wote wanapatikana tunafanya hivyo ili kurahisisha shughuli zetu kwa kuwezesha ratiba ya bunge na shughuli ziende kama zilivyo katika mpango wa ratiba za bunge.

“Ni matumaini yangu kuwa kamati zote kwa kushirikiana na Mawaziri wote mtakuwa na mjadala mzuri na ambapo mtahitaji kuuliza jambo lolote mawaziri wataweza kutoa ufafanuzi na majibu yatapatikana kwa wakati na serikali itapokea ushauri utakaotolewa na kamati na utafanyiwa kazi,” alisema Majaliwa.

Naye Spika wa Bunge, Job Ndugai alisema kuwa anaielekeza kamati ya Bajeti mara baada ya mkutano wa kuwasilisha Mapendekezo ya Bajeti ya Fedha ua mwaka 2019/20 ianze mara moja kuyafanyia uchambuzi mapendekezo yaliyo wasilishwa na kuanza kuzishauri kamati za Bunge za kisekta pamoja na kuanza kuishauri serikali kuhusu mapendekezo hayo.

“Kwa mujibu wa kanuni ya 98 kanuni ndogo ya pili kabla ya kuanza mkutano wa bajeti kamati za bunge za kisekta zitapata fursa ya kuchapisha taarifa za utelelezaji wa bajeti za Wizara zinazosimamia yaani wizara ambazo kamati hizo zinasimamia kamati maalumu ndani ya kamati hizo kwa ajili ya kufanya uimarisho kuhusu makadirio ya mapato na matumizi ya serikali kwa mwaka wa fedha ujao.

“Ili kamati ziweze kutekeleza majukumu hayo natoa rai kwa serikali kuhakikisha kuwa nyaraka zote zinazotakiwa kuwepo kwenye kamati zinazohusika zinawasilishwa kwa wakati,” alisema Ndugai.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Tume huru ya uchaguzi yatangaza ajira watendaji daftari wapiga kura

Spread the love  TUME Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), imetangaza nafasi...

Habari za SiasaTangulizi

Chadema yatangaza ruti awamu ya pili maandamano

Spread the love  CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimesema awamu ya...

Habari za Siasa

CCM yamkana mwenyekiti UVCCM aliyetaka wapinzani wapotezwe

Spread the love  CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimejitenga na kauli ya mwenyekiti...

Habari za SiasaTangulizi

Rais Samia kutunukiwa udaktari wa heshima Uturuki

Spread the loveBaraza la Chuo Kikuu cha Ankara, ambacho ni cha pili...

error: Content is protected !!