Monday , 30 January 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Kubenea ang’ata na kupuliza mpango wa Maendeleo ya Taifa
Habari za Siasa

Kubenea ang’ata na kupuliza mpango wa Maendeleo ya Taifa

Saed Kubenea, Mbunge wa Ubungo
Spread the love

MBUNGE wa Jimbo la Ubungo, Saed Kubenea (Chadema) amesema kuwa mpango uliowasilishwa leo na Waziri wa Fedha na Mipango kwa wabunge wote wa kamati za kudumu za bunge kuwa ni mzuri. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma … (endelea).

Muda mfupi baada ya kuwasilishwa kwa mapendekezo ya ya serikali  ya mpango wa maendeleo wa taifa na ya  kiwango cha ukomo wa Bajeti ya serikali kwa mwaka wa fedha kwa mwaka wa fedha 2019/20 ambacho serikali inakusudia kutumia kiasi cha Sh. 33,105.4 trilioni.Kubenea alisema kuwa ni mpango mzuri japo unaweza kushindwa kutekelezeka.

Akizungumza na MwanaHALISI ONLINE alisema kuwa kwa ujumla wake mpango uliowasilishwa na serikali ni mzuri kwa sababu ni mpango wa muda mrefu na muda mfupi.

Alisema kuwa pamoja na kuwa mpango huo kuwa mzuri lakini shida ambayo kwa sasa anaiona katika kipindi cha miaka miwili iliyobakia kabla ya uchaguzi mkuu serikali imechukua miradi mingi na mikubwa ambayo uwezekano wa kukamilika kwa muda mfupi cha miaka mitatu au minne ni kifupi.

Alisema kuwa miradi hiyo mingi inaendeshwa na fedha  za ndani na mapato ya ndani ya kodi siyo makubwa.

Alisema kuwa mapato ya ndani hayazidi Sh. 20 trilioni kwa hiyo utekelezaji wa miradi mikubwa kama ujenzi wa reli ya kati, ujenzi wa bwawa la umeme la Rufiji, barabara, ununuzi wa ndege, upanuzi wa viwanja vya ndege ni miradi mikubwa.

“Serikali ingeweza kutengeneza utaratibu mzuri wa kufanya maelewano mazuri na nchi na nchi wahisani na nchi wahisani wangeweza kusaidia.

“Nitoe mfano mdogo wa barabara ya Morogoro kutoka Kimara hadi Kibaha ambayo ni ya njia nane, barabara ile ilipata fedha kutoka benki ya Dunia na ni mkopo uliokuwa wa masharti nafuu lakini benki ya dunia ilitoa sharti kwamba serikali ilipe fidia wale waathirika maeneo yale ambayo barabara inapita.

“Sasa serikali ilikataa kulipa fidia na benki ya dunia ikajiondoa katika ule mradi sasa ukiangalia fedha inayotumika ni nyingi sana katika  ujenzi wa ile barabara kuliko kwamba uengeenda kuomba ule mkopo ambao ungeweza kulipa watu fidia alafu ukaweza kuendesha huo mradi.

“Sasa miradi kama hiyo iko mingi kwa hiyo mimi kwa maoni yangu mpango ni mzuri lakini serikali imebeba mambo mengi na inataka kuyatekeleza kwa wakati mmoja na kwa haraka sana jambo ambalo nadhani tunaweza tukafika mahala tukakwama lakini la pili kuna miradi ambayo ilikuwa ikitekelezwa na kufikia hatua nzuri sana wakati wa utawala uliopita kwa mfano mradi wa gesi wa Mtwara na kwa kipindi cha miaka tatu serikali ya awamu ya tano ikauwacha ule mradi kama imeusahau na sasa hivi ndipo imeuleta katika mpango kwamba uchakataji wa gesi, wanazungumzia Mchuchuma, Liganga wanazungumzia kwa hiyo ni miradi ambayo ingekuwa imeendelezwa leo tungekuwa tumefika katika hatua nzuri sana na sasa tunaelekea katika uchaguzi mkuu wa serikali za mitaa uchaguzi mkuu na pesa zinazotakiwa ni nyingi sana,” alisema Kubenea.

Kwa upande wake Mbunge wa Same Mashariki, Naghenjwa Kaboyoka alisema kuwa Tanzania ni bingwa wa kuwa na mipango mizuri lakini utekelezaji ni tatizo.

Alisema kuwa imefika hatua ambayo inawezekana watendaji wa serikali wamekuwa na nia ya kukwamisha juhudi za serikali katika hali ya kimaendeleo.

Alisema inashangaza kuona wakandarasi wanaotengeneza barabara wamekuwa wakisubiri kipindi cha mvua ndipo wanaanza kutengeneza barabara.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Chongolo asikitishwa na mradi wa Mil 900 kutoanza kutoa manufaa

Spread the loveKATIBU mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa Daniel Chongolo...

Habari za Siasa

NCCR-mageuzi yawaangukia Polisi kupotea kwa kada wake

Spread the loveJESHI la Polisi nchini limeombwa kufanya uchunguzi wa kina utakaosaidia...

Habari za Siasa

Uamuzi kesi ya kupinga Bodi ya Wadhamini NCCR-Mageuzi kutolewa Februari 6

Spread the love  MAHAKAMA Kuu, Masjala Kuu ya Dar es Salaam, imepanga...

Habari za SiasaTangulizi

Lissu:Suluhu ya ugumu wa maisha ni Katiba Mpya

Spread the love  MAKAMU mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo-Chadema Bara,...

error: Content is protected !!