Thursday , 9 May 2024
Home Kitengo Michezo Mchezaji Yanga afungiwa mechi tatu
Michezo

Mchezaji Yanga afungiwa mechi tatu

Clifford Ndimbo, Msemaji wa TFF
Spread the love

BEKI wa klabu ya Yanga Abdallah Shaibu ‘Ninja’ amefungiwa michezo mitatu baada ya kukutwa na hatia ya kumpiga kiwiko mchezaji Andrew Simchimba kwenye mchezo dhidi Coastal Union uliochezwa 3 februari, 2019. Anaripoti Kelvin Mwaipungu… (endelea)

Mchezaji huyo ambae alihojiwa na kamati ya nidhamu hapo jana alikili kosa hilo na kusema haikuwa dhamila yake bali alikuwa akijaribu kumzuia asipite hivyo kamati ikaamua kumsimamisha michezo mitatu mfululizo.

Afisa Habari wa shirikisho la mpira Tanzania TFF Clifford Ndimbo ameeleza kuwa Kamati hiyo ambayo ilikutana  jana jumapili chini ya mwenyekiti wake wakili Kiomoni Kibamba.

“Kamati imempa adhabu ya kufungiwa kutocheza michezo mitatu mfululizo kwa mujibu wa kifungu cha 48(1) (d) cha kanuni ya nidhamu” alisema Ndimbo

Hapo awali mcherzaji huyo aliitwa na kamati ya nidhamu ya shirikisho la mpira wa miguu nchini Tff na kushindwa kutokea kutokana na timu yake kuwa katika michezo mikoani.

Ninja ambae kwa sasa amekuwa mchezaji muhimu kwenye kikosi cha Yanga ataikosa michezo dhidi ya Lipuli Fc, Ndanda na African Lyon.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoMichezo

Kengold wakabidhiwa kombe NBC Championship

Spread the loveMdhamini mkuu wa Ligi Daraja la Kwanza (NBC Championship) Benki...

Michezo

Piga pesa na mechi za UEFA

Spread the love  HATIMAYE leo hii ndio kitaeleweka nani aende Nusu Fainali...

Michezo

Idris Sultan anogesha msimu wa 3 wa Bridgerton

Spread the loveSTAA wa burudani kutoka ardhi ya Tanzania, Idris Sultan amenogesha...

Michezo

Ligi mbalimbali za pesa kuendelea leo

Spread the love JUMAPILI ya leo imekaa kipesa tuu yani baada ya...

error: Content is protected !!