Friday , 29 September 2023
Home Gazeti Habari za Siasa UVCCM wamnanga Lowassa
Habari za SiasaTangulizi

UVCCM wamnanga Lowassa

Edward Lowassa, Waziri Mkuu Mstaafu
Spread the love

WAKATI wengine wakimtete Edward Lowassa, aliyekuwa mgombea urais kupitia Chadema kwenye Uchaguzi Mkuu 2015 na kuamua kuhamia CCM tarehe 1 Machi 2019, Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) waanza kumsigina. Anaripoti Dany Tibason…(endelea).

UVCCM imempokea Lowassa, aliyewahi kuwa Waziri Mkuu lakini imempa masharti kwamba, akae kimya kuzingatia, kutafakari na kuyaishi matakwa ya chama hicho na si vinginevyo.

Umoja huo umeeleza kuwa, kurejea kwa Lowassa hakuwezi kutafsiriwa kuwa ni dhambi ila kinachotakiwa ni kukaa kimya ili aendelee kuwa mwanachama wa chama hicho baada ya kupokewa.

Mbali na hilo UVCCM wameeleza kwamba, Lowassa hakuombwa kurejea CCM bali yeye mwenyewe na ndiye aliyeomba na kwamba, taratibu za kumfikiria na kumjadili zilifanywa ikiwa ni pamoja na kumtaka kujieleza na kukiri makosa aliyoyafanya akiwa mwanachama wa CCM.

Khery James, Mwenyekiti wa UVCCM akizungumza na waandishi wa habari leo tarehe 11 Machi 2019 jijini Dodoma amesema, kwa sasa Lowassa anachukuliwa kama mwanachama mpya ndani ya chama hicho na ndiyo maana alipewa kadi mpya na siyo ile ya zamamni aliyokuwa akiimiliki.

Amesema, Lowassa pamoja na kurejea CCM lakini ni lazima akubali kusikiliza kile ambacho kinatakiwa ndani ya chama kwa kufuata misingi, kanuni na taratibu ndani za chama husika na si viginevyo.

Amesema, CCM ina maadili yake na si chama ambacho mtu anaweza kuingia na kujichukulia uamuzi wake mwenyewe.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Kapinga: Usambazaji umeme vijijini mwisho Desemba 2023

Spread the love  NAIBU Waziri wa Nishati, Judith Kapinga, amesema ifikapo mwezi...

Habari za Siasa

Mgongano wa kimasilahi wamhamisha Chande TTCL

Spread the love  ALIYEKUWA Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO),...

Habari za SiasaTangulizi

Mgawo wa umeme: Rais Samia ampa miezi sita bosi mpya TANESCO

Spread the love  RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amempa miezi sita Mkurugenzi...

Habari za Siasa

Rais Samia avunja bodi ya REA

Spread the loveRAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amemteua Balozi Jacob Kingu, kuwa...

error: Content is protected !!