Saturday , 27 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Kifo kilivyokatisha mpango wa Rais Kikwete kwa Ruge
Habari za SiasaTangulizi

Kifo kilivyokatisha mpango wa Rais Kikwete kwa Ruge

Rais Mstaafu Jakaya Kikwete alipokuwa na Marehemu Ruge Mutahaba
Spread the love

NIA na dhamira ya Rais Mstaafu, Jakaya Kikwete kuwa mlezi wa Ruge Mutahabu, mwanahabari aliyekuwa mtayarishaji wa vipindi vya Clouds Media Group (CMG) yamekatizwa. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Dhamira ya Rais Kikwete kuwa mlezi wa Ruge ilikatishwa na mauti yaliyomfika mwanahabari huyo tarehe 26 Februari 2019 akiwa nchini Afrika Kusini akitibiwa maradhi ya figo.

Katika uhai wake Ruge aliwasiliana na Rais Kikwete kuhusu kuwa mlezi wa programu yake mpya na ya muda mrefu ya ‘Kamata Fursa’ ambayo aliianzisha kwa lengo la kusaidia vijana kujua fursa zinazowazunguka na hatimaye kuzitumia.

Akiwa msibani tarehe 28 Februari 2019 Rais Kikwete alisema, Ruge na timu yake walipoanzisha program ya fursa alishiriki katika kuzindua wake na hapo ndio aliombwa kuwa mlezi.

Kutokana na malengo mazuri ya programu hiyo, Rais Kikwete alisema, alikubaliana na ombi la Ruge kwani Watanzania vijana wengine wangeenda kunufaika na mpango huo.

“Aliniambia kwamba, tutazugumzia hili baadaye. Ndipo nikasikia aliugua, nikasikia alikwenda India na baadaye alipelekwa Afrika Kusini. Kama mara tatu nne hivi nilienda kumtembelea alipokuwa Afrika Kusini,” alisema Kikwete.

Rais Kikwete alisema, alikuwa akivutiwa na Ruge kutokana na shughuli walizokuwa wakizifanya yeye na timu yake “mimi nilikuwa natoa ushauri tu,” amesema.

Rais huyo mstaafu alisema, alimfahamu Ruge kwa miaka 20 iliyopita na aliendelea kuwa naye karibu na kwamba, hata walipokuwa na matatizo yao wenyewe, walimfuata na kuomba msaada.

Miongoni mwa kazi ambazo Ruge alimshirikisha Rais Kikwete ni pamoja na uzinduzi wa Tanzania House Talent (THT).

Kwenye uzinduzi huo wa kuinua vipaji vya wasanii Ruge alimwomba Rais Kikwete awasaidie kupata vifaa vya kufanyakazi kwa ufanisi kwenye chombo hicho.

“Nilipoambiwa Ruge amefariki, nilishtuka sana kwani nilikuwa nimeshapata matumaini baada ya kupata taarifa kwamba, alikuwa ametoka ICU,” alisema Rais Kikwete na kuongeza;

“Taifa limepoteza mzalendo ambaye alikuwa mfano wa watu kwani alikuwa tayari kujitolea kwa ajili ya kuwanufaisha wengine.”

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Sauti ya Watanzania waeleza sababu za kuiunga mkono Chadema

Spread the love  KIKUNDI kinachojipambanua katika kupigania rasilimali na uhuru wa nchi,...

Habari MchanganyikoTangulizi

Jacob, Malisa waachiwa kwa masharti

Spread the love  JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam,...

Habari za SiasaKimataifaTangulizi

Tanzania, Somalia kuibua maeneo mapya ya ushirikiano

Spread the love  RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amesema Tanzania na Somalia...

Habari za Siasa

ACT: Waongoza watalii wapate maslahi yao inavyostahili

Spread the loveCHAMA cha ACT-Wazalendo kimeitaka serikali kuhakikisha inasimamia maslahi stahiki ya...

error: Content is protected !!