Tuesday , 16 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa BREAKING NEWS: Mbowe aibwaga Serikali Mahakama ya Rufaa
Habari za SiasaTangulizi

BREAKING NEWS: Mbowe aibwaga Serikali Mahakama ya Rufaa

Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa Chadema (kulia) akiwa mahakamani Kisutu na Ester Matiko, Mbunge wa Tarime Mjini
Spread the love

MAHAKAMA ya Rufaa ya Tanzania, imetupilia mbali maombi ya Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP), kupinga Mahakama Kuu, kusikiliza maombi ya kurejeshewa dhamana kwa wabunge wawili wa upinzani chini. Anaripoti Faki Sosi … (endelea).

Katika uamuzi wake uliotolewa leo Ijumaa, majaji wa Mahakama ya Rufaa wamesema, Mahakama Kuu ilikuwa sahihi kuendelea kusikiliza shauri hilo, hata kama hakukuwapo mwenendo wa kesi ya jinai iliyoamriwa na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.

Aidha, Majaji wa Mahakama ya Rufaa wameeleza kuwa DDP alikosea kuwasilisha shauri hilo mahakamani hapo, wakati shauri la msingi bado linaendelea mahakama kuu.

Katika shauri hili, DDP iliwasilisha hoja mbili za kuomba rufaa Na. 344 iliyopo mbele ya Jaji wa Mahakama Kuu, Sam Rumanyika, iondolewe mahakani hapo.

Akisoma maamuzi hayo ya majaji, Naibu Msajili wa Mahakama ya Rufaa, Silyvester Kainda alisema, majaji wamepitia maombi hayo ya rufaa na wameipa rufaa hiyo uzito mkubwa.

“…ni maoni yetu na msimamo wa Mahakama hii, kwamba waomba rufaa (DPP), hawakuwa na haki yoyote ya kisheria ya kuleta shauri hili Mahakamani. Sisi Majaji wa Mahakama ya Rufaa, tumejiridhisha kuwa waomba rufaa walisikilizwa kikamilifu na jaji wa Mahakama Kuu,” ameeleza Msajili wa mahakama hiyo aliyekuwa anasikiliza shauri hilo.

Alisema, “hii ni kwa sababu, wakati kesi hiyo inaendelea kwenye Mahakama Kuu, Mkurugenzi wa Mashtaka aliwasilisha rufaa Mahakama ya Rufani kwa jambo ambalo liko kwenye mamlaka ya Mahakama.”

Wajibu wa maombi katika kesi hiyo, ni mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) na mbunge wa Tarime Mjini, Esther Matiko.

Shauri hilo lilisiikilizwa na jopo la majaji watatu – Gerald Ndika, Stella Mgasha na Mwanaisha Kwaliko.

Mbowe na Matiko, kupitia mawakili wao, Peter Kibatara na Prof. Abdallah Safari, waliwasilisha Mahakama Kuu, maombi ya kurejeshewa dhamana yao, kufuatia kufutiwa na Mahakama ya Kisutu, tarehe 30 Novemba 2018.

Hakimu Mkuu Mkazi wa Mahakama ya Kisutu, Wilbard Mashauri, kwa alichokieleza kuwa wamekiuka mashart ya dhamana.

Hoja za upande wa serikali juu ya rufaa hiyo, ni pamoja na Mahakama Kuu kutotoa muda wa kuwasikiliza wakati wa usikilizwaji wa rufaa ya Mbowe na Matiko.

Katika shauri hilo la jinai, DPP aliwasilishwa na wanasheria wake wawili, Faraja Nchimbi na Paul Kadushi.

Wote kwa pamoja, aliwasilisha hoja zilizolenga kuiomba mahakama kuiondoa rufaa ya Mbowe na Matiko kwa madai kuwa haina miguu ya kisheria na kinyume cha sheria ya mwenendo wa makosa ya jinai.

Nchimbi alidai kuwa Jaji Rumanyika alipotoka kisheria kwa kuipanga na kuiita kwa ajili ya usikilizwaji kesi hiyo, huku akijua kuwa rufaa hiyo iliwasilishwa kinyume na Kifungu cha 362 (1) cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai Sura ya 20 kilichofanyiwa marejeo mwaka 2002.

Naye wakili Kibatala aliileza Mahakama kuwa rufaa hiyo haina mashiko na kuomba kutupiliwa mbali.

Mbowe ambaye pia ni mbunge wa Hai, mkoani Kilimanjaro na Matiko, walifutiwa dhama zao tarehe 23 Novemba 2018, kufuatia Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, kudai kuwa imejiridhisha kwamba wote wawili, walitenda kinyume na masharti ya dhamana walizopewa.

Katika kesi ya msingi, Mbowe, Matiko na watu wengine saba, wanakabiliwa na mashitaka 13, ikiwemo kula njama, kufanya mkusanyiko wenye ghasia, kuhamasisha hisia za chuki, kushawishi hali ya kutoridhika, uchochezi na kushawishi utendaji wa kosa la jinai. Wanadaiwa kutenda kosa hilo, kati ya 1 Februari na 16 Machi, mwaka jana, maeneo ya Dar es Salaam.

Washitakiwa wengine kwenye kesi hiyo, ni Katibu Mkuu wa Chadema, Dk. Vincent Mashinji; Mbunge wa Iriga Mjini, Mchungaji Peter Msigwa na Mbunge wa Kibamba na Katibu wa Chadema, Tanzania Bara, John Mnyika.

Wengine, ni Mbunge wa Bunda Mjini, Ester Bulaya, Mbunge wa Kawe na Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake la chama hicho (BAWACHA), Halima Mdee; Mbunge wa Tarime Vijijini, John Heche na Naibu Katibu Mkuu (Zanzibar), Salum Mwalimu.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Samia arejesha mikopo ya 10%, bilioni 227.96 zatengwa

Spread the loveRAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amerejesha utaratibu wa utoaji mikopo...

Habari za Siasa

Rais Samia amfariji mjane wa Musa Abdulrahman

Spread the loveRais Samia Suluhu Hassan leo Jumanne amempa pole Mwanakheri Mussa...

Habari za Siasa

Nape: Wanasiasa, wanahabari, wafanyabiashara mteteeni Samia

Spread the loveWaziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari na Mawasiliano,...

Habari za Siasa

CAG: TAWA imegawa vibali vya uwindaji bila idhini ya waziri

Spread the loveRIPOTI ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali...

error: Content is protected !!