Tuesday , 30 May 2023
Home Kitengo Maisha Elimu Serikali yatangaza ajira za walimu 4,500
Elimu

Serikali yatangaza ajira za walimu 4,500

Spread the love

SERIKALI imetangaza kuajiri walimu 4,549 wa shule za msingi na sekondari katika mwaka wa fedha 2018/19 ili kupunguza uhaba wa walimu ulipo nchini. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma … (endelea).

Aidha, ajira hizo mpya waombaji watapaswa kuomba kwa njia ya mtandao na mwisho wa kupokea maombi utakuwa Machi 15, mwaka huu.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Seleman Jafo aliyasema hayo jana wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari jijini hapa.

Alisema serikali inatambua changamoto zilizopo katika sekta ya elimu nchini ikiwemo uhaba wa walimu na itaajiri walimu hao ili kupunguza uhaba huo.

“Mheshimiwa Rais John Magufuli, anaendelea na kuongeza idadi ya watumishi katika sekta ya Umma kwa kutoa nafasi zingine za ajira kwa vijana wa kitanzania katika sekta ya Elimu…mchakato huu wa sasa wa ajira utahusisha ajira mpya za watumishi 4,549 ambazo zitahusisha walimu wa shule za msingi na sekondari,” alisema Jafo.

Aidha Jafo alisema kuwa kwa sababu hiyo Ofisi ya Rais Tamisemi inawatangazia walimu wenye sifa kutuma maombi yao kwa njia ya mtandao (Online Teacher Employment Application System-OTEAS).

Alisema kwa walimu wa shule za msingi wanaotakiwa kutuma maombi ni wenye sifa za kitaaluma Daraja la IIIA wenye Astashahada ya ualimu, na wenye daraja la IIIB wenye Stashada (Diploma ya ualimu katika masomo ya English, Civics, Historia, Jiografia na kiswahili.

Aliongeza kuwa walimu wengine ni wale wenye sifa ya Daraja la IIIC wenye shahada ya ualimu kwa masomo ya English,Civics, General Studies, History, Geography na Kiswahili.

Vilevile alisema kundi jingine lenye sifa ni mwalimu mwenye Daraja la IIIC na mwenye mahitaji maalum aliyehitimu Shahada kwa masomo ya English, Civics, General studies, History, Geography na kiswahili.

Kwa walimu wa sekondari Jafo alisema wanaotakiwa kufanya maombi ni mwalimu wenye Daraja la IIIC mwenye Shahada ya ualimu aliyesomea Elimu maalum.

Wengine ni wale wenye Daraja la IIIB wenye Stashahada (Diploma) ya ualimu waliosomea Elimu maalum na mwalimu Daraja la IIIB mwenye Stashahada ya ualimu somo la Physics, Mathematics, Biology na Chemistry.

“Wengine wenye sifa za kuomba ni mwalimu daraja la IIIC mwenye shahada ya ualimu somo la Agriculture Science, na mwalimu wa Daraja la IIIC mwenye Shahada ya ualimu somo la Home Economics na mwalimu Daraja IIIC mwenye Shahada ya ualimu somo la Physics, Mathematics, Chemistry na Biology,” alisema Jafo.

Aliongeza kuwa walimu wengine ni wale wa Daraja IIIC wenye shahada ya ualimu somo la Book keeping, Commerce, Acconts na Economics na mwalimu daraja la IIIC mwenye Shahada ya ualimu somo la English, Civics na General Studies.

Jafo alifafanua kuwa waombaji wenye sifa zote hizo wanatakiwa kuwa watanzania, wawe wamehitimu kati ya mwaka 2014 hadi 2017 isipokuwa kwa kundi maalum la wahitimu wa elimu ya ualimu wa masomo ya fizikia na hisabati.

Sifa nyingine ya jumla alisema ni muombaji asiwe na umri zaidi ya miaka 45, na wakati wa kutuma maombi walimu ambao waliwahi kutuma na hawajaajiriwa wanapaswa kutuma upya.

Katika hatua nyingine Jafo amewataka viongozi wa Kisiasa kuwaheshimu watumishi wa Umma na kuacha kuwadhalililisha hadharani hali inayochangia kuwavunja moyo katika utendaji wao.

Alisema Viongozi hao wanatakiwa kuwaheshimu watumishi wa Umma na kuacha kuwadhalilisha hadharani kwani hali hiyo ni kinyume na maadili ya utumishi wa Umma.

“Sisemi kuwa hakuna watumishi wenye mapungufu, la hasha ninachotaka mimi utaratibu ufuatwe katika kuwaadhibu si kuwadhalilisha hadharani,” alisema Jafo.

Alisema mfano wa tukio moja lililotokea huko mkoani Tanga la mtumishi kudaiwa kudhalilishwa halifurahishi na linawavunja moyo watu wengine.

“Sipendezwi sana kama kuna vitendo vya uzalilishaji kwani viwawavunja moyo wengine, naomba kama kuna mtumishi amekosa viongozi watumie utaratibu wa kiutumishi kwa kufuata hatua za kiutawala,” alisisitiza Jafo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Elimu

SUA kuhakikisha tafiti zinazofanywa zisiachwe kwenye makabati

Spread the love  MRATIBU wa utafiti na machapisho katika kurugenzi ya uzamiri,...

Elimu

Watakaopata Division One St Anne Marie Academy kupewa iphone ya macho matatu

Spread the loveMkurugenzi wa shule za St Anne Marie Academy, Dk. Jasson...

Elimu

Prof. Muhongo apinga TAMISEMI kusimamia elimu

Spread the love  MBUNGE wa Musoma Vijijini, Prof. Sospeter Muhongo, ameshauri masuala...

Elimu

SUA kuboresha ufundishaji kupambania ajira za wahitimu

Spread the love  CHUO kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) mkoani hapa...

error: Content is protected !!