Tuesday , 7 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Mbunge CCM alikoroga, wananchi wamjia juu
Habari za SiasaTangulizi

Mbunge CCM alikoroga, wananchi wamjia juu

Spread the love

EMMANUEL Papian, Mbunge wa Kiteto kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) amejikuta kwenye wakati mgumu baada ya kuukana ukweli mbele ya kadamnasi. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Mbele ya timu ya mawaziri wanane wanaozunguka maeneo mbalimbali nchini kutatua migogoro ya ardhi, walipofanya mkutano wao Kiteto, Manyara mbunge huo aliwaambia kuwa, katika Kijiji cha Ilkiushbour hakuna mtu aliyepigwa risasi na polisi wala kugongwa na gari kwama ilivyoelezwa na Melubo Naiganya, Mwenyekiti wa Kijiji cha Ilkiushbour.

Taarifa ya mbunge huyo ilizua zomeazomea baada ya kupingana na ile ya mwenyekiti Naiganyailiyoeleza kuwa, watu wawili wamefikwa na majanga ambapo mmoja alipigwa risasi huku mwingine akigongwa na gari.

Naiganya alitoa taarifa hiyo mbele ya Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi; Waziri wa Maji, Profesa Makame Mbarawa; Naibu Waziri wa Kilimo, Omari Mgumba na Waziri wa TAMISEMI, Selemani Jafo.

Mawaziri wengine waliokuwepo ni pamoja na Waziri wa Ulinzi, Dk. Husein Mwinyi; Waziri wa Maliasili, Hamis Kigwangala Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina ambapo mawaziri hao walifika katika Kijiji cha Kimotorok kutatua kero na hifadhi ya Kiteto.

Mbele ya mawaziri hao tarehe 26 Februari 2019 Mbunge Papian alikana taarifa iliyotolewa ya mwenyekiti wa kijiji hicho –Naiganya- kwamba haina ukweli wowote.

Alisema, hakuna mwananchi alipigwa risasi na wala aliyegongwa na gari la pori la Akiba la Mkungunero.

“Mmoja aliangukia sime na mwingine alianguka wakati akifukuzana na askari polisi,” alisema mbunge huyo kauli ambayo ilipandisha hasira za wananchi na kumtaka aombe radhi.

Kutokana na taarifa ya mbunge huyo, wananchi walisema kuwa amepotosha ukweli na kumtaka akane ama kufuta kauli hiyo ya kwamba, hakuna mtu aliyepigwa risasi wa kama kugongwa na gari.

Hata hivyo, mwenyekiti Naiganya alisema kuwa, Mathayo Urumjee aligongwa na gari wakati Atabai Kuya alipigwa risasi na kwamba, taarifa hizo waliripoti polisi.

“Aliyepigwa risasi tulimpeleka katika Hospitali ya Rufaa Dodoma ili apatiwe matibabu,” amesema na kuongeza kwamba, aliyegongwa na gari anahitaji msaada zaidi kwa kuwa hali yake bado mbaya.

Amesema, kutokana na kushindwa kugharamia matibabu Urumjee amelazimika kurejeshwa nyumbani ambapo mwenyekiti huyo ameomba serikali kumtibu.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Rais Samia ni Mzanzibari: Shida Iko Wapi?

Spread the loveTAIFA linakabiliwa na upungufu wa fikra sahihi. Upungufu huu unaonekana...

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Mpina mwiba CCM, ahofia kuzibwa mdomo

Spread the loveWAKATI Chama cha Mapinduzi (CCM), kikijinasibu kuwa kinara wa demokrasia...

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Mabeyo ametuepusha

Spread the loveNIMEGUSWA na uadilifu, utiifu na uaminifu wa Mkuu mstaafu wa...

Habari za SiasaTangulizi

CCM yaitaka TAKUKURU kuichunguza Chadema tuhuma alizoibua Lissu

Spread the loveCHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimeitaka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana...

error: Content is protected !!