SALAMU za majonzi za watu mbalimbali mashuhuri wakiwemo viongozi wa serikali, vyama vya siasa na wasanii zimeendelea kuelekekezwa kwa Familia ya Mwanahabari mashuhuri nchini Ruge Mutahaba aliyefariki dunia jana tarehe 27 Februari 2019. Anaripoti Faki Sosi … (endelea).
Ruge aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Vipindi wa Clouds Media Group, alifariki dunia jana nchini Afrika Kusini alikokuwa anapatiwa matibabu ya tatizo la figo lililomsumbua kwa zaidi ya miezi minne, ambapo alianza kutibiwa katika Hospitali ya Kairuki iliyoko jijini Dar es Salaam, na baadae akapelekwa India kisha kupelekwa Afrika Kusini ambako umauti ulimfika.
Miongoni mwa viongozi wa ngazi za juu wa nchi na wanasiasa waliotoa salamu za pole kufuatia kifo cha Ruge ni pamoja na Rais John Magufuli, ambaye kupitia ukurasa wake wa Twitter jana aliandika kuwa: “Nimepokea kwa masikitiko taarifa za kifo cha kijana wangu Ruge Mutahaba. Daima nitamkumbuka kwa mchango wake mkubwa ktk tasnia ya habari, burudani, na juhudi za kujenga fikra za maendeleo kwa vijana. Poleni wanafamilia,ndugu,jamaa na marafiki. Mungu amweke mahali pema, Amina.”
Nimepokea kwa masikitiko taarifa za kifo cha kijana wangu Ruge Mutahaba. Daima nitamkumbuka kwa mchango wake mkubwa ktk tasnia ya habari, burudani, na juhudi za kujenga fikra za maendeleo kwa vijana. Poleni wanafamilia,ndugu,jamaa na marafiki. Mungu amweke mahali pema, Amina.
— Dr John Magufuli (@MagufuliJP) February 26, 2019
Rais Mstaafu Jakaya Kikwete ameandika kwenye ukurasa wake Twitter: “Nimelemewa! Nakosa maneno ya kuelezea huzuni na majonzi niliyonayo kwa kifo cha Ruge Mutahaba. Taifa limepoteza kijana wake mahiri, mbunifu na mzalendo wa kweli. Nimepoteza rafiki, mshirika mwaminifu na mtu ambaye amenisaidia kwa mengi ktk uongozi wangu na hata baada ya kustaafu.”
Nimelemewa! Nakosa maneno ya kuelezea huzuni na majonzi niliyonayo kwa kifo cha Ruge Mutahaba. Taifa limepoteza kijana wake mahiri, mbunifu na mzalendo wa kweli. Nimepoteza rafiki, mshirika mwaminifu na mtu ambaye amenisaidia kwa mengi ktk uongozi wangu na hata baada ya kustaafu. pic.twitter.com/oBqoWBQF8T
— Jakaya Kikwete (@jmkikwete) February 26, 2019
Makamu wa Rais, Mama Samia Suluhu Hassan katika ukurasa wake wa Twitter ameandika kuwa: “Umewafungulia Dunia mamia ya Vijana nchini, umekuwa mbunifu na mtambuzi wa fursa mbalimbali, Hakika tumepoteza Shujaa na Mpiganaji mahiri. Pumzika kwa amani Ruge.”
Umewafungulia Dunia mamia ya Vijana nchini, umekuwa mbunifu na mtambuzi wa fursa mbalimbali, Hakika tumepoteza Shujaa na Mpiganaji mahiri. Pumzika kwa amani Ruge.
— Samia Suluhu (@SuluhuSamia) February 26, 2019
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais-Mazingira na Muungano, January Makamba katika akaunti yake ya Twitter ameandika “ Ruge. Ruge. Ruge. Nakosa maneno ya kutosheleza kuelezea maumivu na huzuni niliyonayo. Kwa sasa, dua na fikra zangu ni kwa Mama, Dkt. Mutahaba, ndugu na marafiki ambao walihangaika sana kuhakikisha anapona. Nikipata nguvu nitasema zaidi. Tangulia jamaa yangu, tunakuja. #RIPRuge.”
Ruge. Ruge. Ruge. Nakosa maneno ya kutosheleza kuelezea maumivu na huzuni niliyonayo. Kwa sasa, dua na fikra zangu ni kwa Mama, Dkt. Mutahaba, ndugu na marafiki ambao walihangaika sana kuhakikisha anapona. Nikipata nguvu nitasema zaidi. Tangulia jamaa yangu, tunakuja. #RIPRuge
— January Makamba (@JMakamba) February 26, 2019
“Pumzika kwa Amani kaka! Huna mfano wako duniani, maisha yako yameacha alama kubwa, utaishi milele kwa wema wako! Ndugu, Rafiki na Mzalendo wa kweli!,” ameandika Mbunge wa Mtama Nape Nnauye katika ukurasa wake wa Twitter.
Pumzika kwa Amani kaka! Huna mfano wako duniani, maisha yako yameacha alama kubwa, utaishi milele kwa wema wako! Ndugu, Rafiki na Mzalendo wa kweli! pic.twitter.com/VdsTrMgQiF
— Nape Moses Nnauye (@Nnauye_Nape) February 26, 2019
Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe ameelezea majonzi yake kupitia ukurasa wake wa Twitter akiandika kuwa, maisha ya Ruge enzi za uhai wake ni mafunzo kwa waliobakia hai duniani.
“Sisi sote ni wa Mungu na kwake tutarejea. Ruge umelala moja kwa moja Lakini maisha yako ni mafunzo kwetu tuliobaki. ” Ameendika Zitto kwenye Ukurasa wake wa Twitter.
Sisi sote ni wa Mungu na kwake tutarejea. Ruge umelala moja kwa moja Lakini maisha yako ni mafunzo kwetu tuliobaki. pic.twitter.com/eT5LPfOBj1
— Zitto MwamiRuyagwa Kabwe (@zittokabwe) February 26, 2019
Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi CUF, Maalim Seif Shariff Hamad ameandika kwenye ukurasa wake wa Twitter: “Nimepokea kwa huzuni kubwa taarifa za kifo cha Ruge Mutahaba, kijana aliyetoa mchango mkubwa katika uendelezaji wa fani ya habari Tanzania na kukuza vipaji vya vijana wengine. Kwa niaba ya #CUF nawapa pole familia, ndugu, jamaa, marafiki na Watanzania wote kwa msiba huu mkubwa.”
Nimepokea kwa huzuni kubwa taarifa za kifo cha Ruge Mutahaba, kijana aliyetoa mchango mkubwa katika uendelezaji wa fani ya habari Tanzania na kukuza vipaji vya vijana wengine. Kwa niaba ya #CUF nawapa pole familia, ndugu, jamaa, marafiki na Watanzania wote kwa msiba huu mkubwa. pic.twitter.com/hkY0loAjSr
— Seif Sharif Hamad (@SeifSharifHamad) February 26, 2019
“Najua ya kuwa waweza kufanya mambo yote, Na ya kuwa makusudi yako hayawezi kuzuilika” Ayubu 42:2… “ameandika Mwigulu Nchemba.
Umeondoka Ruge Mtahaba, Umeondoka Shujaa, Umeondoka Mpambanaji. Pole kwa familia,ndugu na Jamaaa, Pole zaidi kwa watanzania wote kwa msiba huu mzito.
"Najua ya kuwa waweza kufanya mambo yote, Na ya kuwa makusudi yako hayawezi kuzuilika" Ayubu 42:2
Amen pic.twitter.com/MkKNDF48vA
— Mwigulu Nchemba, PhD (@mwigulunchemba1) February 26, 2019
Mkurugenzi Mtendaji wa IPP Media, Reginald Mengi naye ametoa salamu zake za pole kwa familia ya Ruge kwa kuandika “RIP Ruge Mutahaba. When you are happily settled in our Lords home, don’t forget your profession. I know and believe you are sufficiently innovative and I am sure you will find a way to communicate with us. Poleni sana familia ya Ruge Mutahaba , wanahabari na watanzania wote.”
RIP Ruge Mutahaba. The Media fraternity is shocked by the very sad news of your untimely departure. You leave behind a huge gap which we shall find very difficult to fill. You were truly a gentleman and pioneer in many aspects of the media. Farewell our Brother.
— Dr Reginald Mengi (@regmengi) February 26, 2019
“RIP Brother Ruge Mutahaba. Our proffession will treasure the legacy which you have left behind!” Ameendika Navile Meena Katibu wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF).
RIP Brother Ruge Mutahaba. Our proffession will treasure the legacy which you have left behind! pic.twitter.com/Rg9CQpsyY4
— Neville Meena (@NevilleMeena) February 26, 2019
Leave a comment