Friday , 29 September 2023
Home Kitengo Habari Kimataifa Rais Buhari ashinda uchaguzi Nigeria
Kimataifa

Rais Buhari ashinda uchaguzi Nigeria

Spread the love

RAIS wa Nigeria, Muhamadu Buhari ameshinda katika matokeo ya awali ya kinyang’anyiro cha uchaguzi wa urais uliofanyika Jumamosi ya tarehe 23 Februari 2019 nchini humo, kwa kupata kura milioni 15. Inaripoti Mitandao ya Kimataifa … (endelea).

Kwa mujibu wa matokeo yaliyotangazwa na Tume Huru ya Kitaifa ya Uchaguzi Nigeria (INEC), Buhari amemzidi kura zaidi ya milioni 4 aliyekuwa mpinzani wake wa karibu, Atiku Aboubakar aliyeambulia kura milioni 11.

Hata hivyo, upinzani nchini Nigeria umeyakataa matokeo hayo. Katika matokeo hayo, chama cha Rais Buhari kimeshinda majimbo 19 kati ya 36 huku chama kikuu cha upinzani nchini humo cha PDP kikishinda majimbo 17.

INEC  imeahidi kuyafanyia kazi malalamiko yote ya wapinzani kabla ya kutangaza rasmi matokeo hayo ya uchaguzi.

Asilimia 35 kati ya watu 73 milioni waliojiandikisha kupiga kura walijitokeza kupiga kura katika uchaguzi huo.

Kama INEC haitabadilisha matokeo hayo, Rais Buhari aliyeingia madarakani tangu mwaka 2015 ataongoza tena Nigeria kwa muhula wa miaka minne mfululizo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Kimataifa

Mahakama yamkuta na hatia Donald Trump

Spread the love  ALIYEKUWA Rais wa Marekani, Donald Trump, amekutwa na hatia...

Kimataifa

Harusi yageuka msiba 100 wakifariki kwa ajali ya moto

Spread the love  WATU takribani 100, akiwemo bibi na bwana harusi, wamefariki...

Kimataifa

Kampuni ya mali ya China Oceanwide yapata agizo la kufilisiwa huko Bermuda

Spread the love  MAHAKAMA ya Bermuda imetoa amri ya kufilisiwa kwa Kamapuni...

Kimataifa

Uvamizi wa kijeshi Milango ya bahari ya Taiwan G7 yapinga China

Spread the loveMKUTANO wa Mawaziri wa Mambo ya nje wa nchi za...

error: Content is protected !!