Tuesday , 30 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Kubenea aikalia kooni Serikali Muswada wa Vyama vya Siasa
Habari za Siasa

Kubenea aikalia kooni Serikali Muswada wa Vyama vya Siasa

Saed Kubenea, Mbunge wa Ubungo
Spread the love

MBUNGE  wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), katika jimbo la Ubungo, Saed Kubenea, amewavaa vigogo watatu ambao ni wanasheria nguli nchini kwa kupeleka muswaada wa sheria ya vyama vya siasa bungeni, wakati unavunja Katiba ya Nchi. Anaripoti Danson Kaijage kutoka Dodoma…(endelea).

Akizungumza bungeni jioni hii, Kubenea amesema, “muswada wa marekebisho wa vyama vya  siasa wa mwaka 2018, unavunja Katiba. Lakini muswaada huu, umeandaliwa na Waziri wa Katiba na Sheria, Prof. Palamagamba Kabudi;  Mwasheria Mkuu wa Serikali (AG), Prof. Adelardus Kilangi na Msajili wa Vyama vya Siasa, Jaji Francis Mtungi.”

Alisema, “sisi tusio wanasheria tunaona vifungu vinavyopingana na sheria. Tuliwaambia kuwa rais atapoteza vyeo vyake kwenye muswada huu lakini wanachama wote wanaweza kupoteza uanachama lakini sio Rais.”

Amesema, muswaada huo haukupitia Baraza la Vyama vya Siasa na kwamba mwenyekiti wa baraza hilo, John Magale Shibuda, alimshukuru Spika wa Bunge, Job Ndugai, kuwaalika katika mjadala wa muswaada.

Kwa mujibu wa Kubenea, muswaada ulioletwa bungeni unamgeuza msajili wa vyama kuwa mlalamikaji, mwendesha mashitaka, jaji na bawana jela.

Kusikiliza mchango kamili wa Kubenea angalia video hapo chini

 

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Mavunde aomba bilioni 231.9 bajeti wizara ya madini

Spread the loveWAZIRI wa Madini, Anthony Mavunde leo Jumanne amewasilisha hotuba ya...

Habari za SiasaTangulizi

Lissu amjibu Fatma Karume kuhusu Rais Samia

Spread the love  MAKAMU Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema)...

Habari za SiasaTangulizi

Dk. Slaa: Watanzania iungeni mkono Chadema uchaguzi 2025

Spread the loveMWANASIASA mkongwe nchini Tanzania, Dk. Wilbroad Slaa, amewataka watanzania wakiunge...

Habari za SiasaTangulizi

Samia ataja miradi ambayo Tanzania inashirikiana na IDA

Spread the loveRais wa Tanzania Dk. Samia Suluhu Hassan leo Jumatatu amehutubia...

error: Content is protected !!