Friday , 19 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Vigogo wa NIDA wasomewa mashtaka 100 Kisutu
Habari Mchanganyiko

Vigogo wa NIDA wasomewa mashtaka 100 Kisutu

Spread the love

DICKSON Maimu aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) na wenzake watano wasomewa mashtaka mapya 100 kwenye Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu pamoja na shitaka na uhujumu Uchumi. Anaripoti Faki Sosi … (endelea).

Washtakiwa wengine ni pamoja na Avelin Momburi, Astery Ndege, George Ntalima, Slivarius Kayombo na Sabini Raymond.

Leo Mbele ya Hakimu Mkasi Salum Ally, wakili wa Serikali Leonard Swai na Simon Wankyo walisoma mashtaka hayo.

Shitaka la kwanza kwenye kesi hiyo namba saba ya Mwaka 2019  kwa mshtakiwa namba moja Maimu ambapo anatuhumiwa kufanya udanganyifu wa kujiingizia pesa kwenye Mamlaka hiyo (NIDA) Sh 1.1 bilioni.

Mshtakiwa namba tatu Ndege anashtikiwa kwenye shitaka la pili, tatu, nne, tano, sita, nane, na tisa.

Pia kwenye shitaka namba 11, 12, 14, 15, 17, 18, 20, 21, 23, 24, 26, 27, 29, 30, 32, 33, 35, 36, 38, 39, 41, 42, 44, 45, 47, 48, 50, 51, 53, 54, 56, 57, 59, 60, 62, 63, 65. Yakiwa ni kughushi nyaraka mbalimbali.

Pia  kuanzia shitaka la 66 hadi 78 mtuhumia amedaiwa kutenda kosa la utakatishaji fedha kiasi cha bilioni.

Lakini mshatakiwa namba moja Maimu na mtuhumiwa namba nne Ntalima amekabiliwa na shtaka namba nne, saba, 10, 13, 16, 22, 25, 28, 31, 34 , 37, 40, 42, 43, 46, 49, 52, 55, 58, 61, 64, wametuhumiwa kughushi nyaraka  kwenye Ofisi za Nida ili kujiingizia dola 10300, (200,854) (14,770), (42600) (118354), Sh. 53 milioni  na zaidi.

Mshtakiwa namba  nne Ntalima ameshitakiwa kwenye shitaka namba 79 hadi 84 kwa kosa la utakatishaji fedha zaidi ya Sh. 50 milioni.

Shitaka namba 85 ni kulagai ambapo mtuhumiwa namba nne Ntalima na namba tano Kayombo  kwa kujiingizia kiasi cha  zaidi ya Sh. 45 milioni.

Shitka la 86 na 87  mtuhumiwa namba nne Ntalima anatuhumiwa kughushi nyaraka kwa kujiingizia zaidi ya Sh. 45 milioni.

Shitaka namba 88 linamkabili Sliverius Kayombo anayedaiwa kujiingizia pesa kwa njia za ulaghai ambapo alijiingizia zaidi ya Sh. 45 milioni. Na  kwenye shitaka namba 89 hadi 93  ni la utakatishaji fedha ambalo linamkabili Kayombo.

Shitaka la 94 Maimu, Ndege na Ntalima wanatuhumiwa kufanya utakatishaji fedha  ambapo kiasia cha Sh. 1.1 bilioni.

Wanadaiwa wakiwa Dar es Salaam kati ya tarehe 19 Julai, 2011 hadi tarehe 31 Agosti 2015 zilizopitishwa kwenye akaunti yenye namba 1408328000 kupitia bank ya CRDB Tawi la Vijana wilayani Ilala.

Shitaka la 95 linamkabili Maimu na Raymond la kutumia vibaya Mamlaka. Shitaka la 96 linamkabili Maimu na Momburi kwa kutowajibika ambapo walipelekea upotevu wa zaidi Sh.40 milioni.

Shtaka la 97 linamkabili Maimu kwa kutowajibika na kusababisha upotevu wa Sh.167,445,671. Na shitaka namba 98 linamkabili Maimu na Ndege kwa kutowajibika kumesababisha hasara ya Sh 1175,785,600.
Shitaka namba 99 linawakabili Ntalima na Kayombo kwa kutowajibika kwao kumesababisha hasara ya zaidi ya Sh.45.

Shtaka la 100 linamkabili Maimu na Raymond kwa kutowajibika kwao kumesababisha hasara ya Sh. 899,935,494.

Watuhumiwa hawakupaswa kujibu chochote kutokana na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu haina mamlaka ya kusikiliza kesi hiyo.

Upande wa serikali umedai kuwa umekamilisha upelelezi na jarada la kesi hiyo limeshawasiliswa mahakama kuu.

Kesi hiyo itatajwa tena terehe 12  Frebruari mwaka 2019.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari Mchanganyiko

Wauguzi, madaktari 1000 kugawiwa mitungi ya Oryx Gas

Spread the loveKAMPUNI ya Oryx Gas na Taasisi ya Doris Mollel Foundation...

Habari Mchanganyiko

Tanzania yachaguliwa Makamu wa Rais Tume ya Shirika la Hali ya Hewa Duniani

Spread the love  TANZANIA kupitia Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA)...

Habari Mchanganyiko

NEMC yaonya wanaojenga bila tathmini ya mazingira

Spread the loveBARAZA la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC),...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB Pesa Akaunti yawavutia wakaguzi wa ndani Afrika

Spread the loveUbunifu wa bidhaa bora wa Benki ya NMB pamoja na...

error: Content is protected !!