MBUNGE wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), katika jimbo la Ubungo, Saed Kubenea, amewavaa vigogo watatu ambao ni wanasheria nguli nchini kwa kupeleka muswaada wa sheria ya vyama vya siasa bungeni, wakati unavunja Katiba ya Nchi. Anaripoti Danson Kaijage kutoka Dodoma…(endelea).
Akizungumza bungeni jioni hii, Kubenea amesema, “muswada wa marekebisho wa vyama vya siasa wa mwaka 2018, unavunja Katiba. Lakini muswaada huu, umeandaliwa na Waziri wa Katiba na Sheria, Prof. Palamagamba Kabudi; Mwasheria Mkuu wa Serikali (AG), Prof. Adelardus Kilangi na Msajili wa Vyama vya Siasa, Jaji Francis Mtungi.”
Alisema, “sisi tusio wanasheria tunaona vifungu vinavyopingana na sheria. Tuliwaambia kuwa rais atapoteza vyeo vyake kwenye muswada huu lakini wanachama wote wanaweza kupoteza uanachama lakini sio Rais.”
Amesema, muswaada huo haukupitia Baraza la Vyama vya Siasa na kwamba mwenyekiti wa baraza hilo, John Magale Shibuda, alimshukuru Spika wa Bunge, Job Ndugai, kuwaalika katika mjadala wa muswaada.
Kwa mujibu wa Kubenea, muswaada ulioletwa bungeni unamgeuza msajili wa vyama kuwa mlalamikaji, mwendesha mashitaka, jaji na bawana jela.
Kusikiliza mchango kamili wa Kubenea angalia video hapo chini
Leave a comment