Wednesday , 8 May 2024
Home Kitengo Michezo Wachezaji Yanga wacheza mechi na njaa, washinda
Michezo

Wachezaji Yanga wacheza mechi na njaa, washinda

Spread the love

WACHEZAJI Yanga wamelazimika kuingia uwanjani kupambana na JKT Tanzania bila kula chakula cha mchana kutokana na mabadiliko ya muda wa mchezo huo. Anaripoti Kelvin Mwaipungu … (endelea).

Mchezo huo wa Ligi Kuu Tanzania Hara awali ulipangwa kuchezwa saa 12 jioni lakini  Bodi ya Ligi ulibadilisha ratiba kuda mchache kabla ya mchezo huo.

Akilalamikia swala hilo Kocha Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera alisema kuwa taarifa ya mabadiliko ya muda katika mchezo wao dhidi ya JKT Tanzania aliyapata saa nne usiku kwa njia ya barua pepe kutoka kwa msemaji wa klabu hiyo Dismas Ten.

“Jana usiku nilipata email (barua pepe) kutoka kwa afisa habari wa timu ikinijulisha kuwa mchezo wetu utakuwa saa 10 jioni badala ya saa 12 jioni kama ulivyopangwa hapo awali, nilishangazwa sana na kujiuliza shirikisho linaweza vipi kufanya mabadiliko ya muda wa mchezo ndani ya mfupi kiasi hicho,” alisema Zahera

Aidha kocha huyo aliongezea kuwa hapo awali walishapanga ratiba yao ya chakula kwa siku ya kesho kuwa watapata kifungua kinywa majira ya saa 5 asubuhi na chakula cha mchana wangekula saa nane mchana

“Wakati napata taarifa hiyo sikuweza kubadilisha utaratibu wa awali kwa kuwa tulishapanga, hivyo sikuweza kuwaamsha wachezaji wangu usiku na kuhusu mabadiliko hayo na kuacha ratiba iendelee vilevile, ilivyofika asubuhi tukapata chai saa 5 asubuhi kama kawaida nakuelekea uwanjani,” aliongezea kocha huyo.

 Licha ya wachezaji kuwa katika hali hiyo lakini walifanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 3-0 ambao umewafanya kuongoza ligi kwa sasa kwa tofauti ya alama moja dhidi ya Azam FC na kubakiwa na rekodi ya kupoteza mpaka sasa katika michezo 14 waliocheza ya Ligi Kuu.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Michezo

Piga pesa na mechi za UEFA

Spread the love  HATIMAYE leo hii ndio kitaeleweka nani aende Nusu Fainali...

Michezo

Idris Sultan anogesha msimu wa 3 wa Bridgerton

Spread the loveSTAA wa burudani kutoka ardhi ya Tanzania, Idris Sultan amenogesha...

Michezo

Ligi mbalimbali za pesa kuendelea leo

Spread the love JUMAPILI ya leo imekaa kipesa tuu yani baada ya...

Michezo

Usiishie kuangalia tu game za leo, piga na mkwanja na Meridianbet

Spread the love  LIGI mbalimbali barani ulaya zitarejea tena Jumamosi ya leo...

error: Content is protected !!