LEO yaweza kuwa siku ngumu kwa utawala na baadhi ya wahadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) iwapo Dk. Vicensia Shule ataamua ‘liwalo na liwe.’ Anaripoti Faki Sosi … (endelea).
Dk. Shule ameitwa mbele ya kamati ya maadili ya chuo hicho baada ya kufikisha ujumbe kwa Rais John Magufuli na Watanzania wote kupitia mtandao wa kijamii (twitter) akieleza namna vitendo vya ngono vinavyotawala chuoni hapo.
Dk. Shule amethibitisha kupigiwa simu na chuo hicho akitakiwa leo mchana kufika mbele ya kamati ya maadili kutokana na ujumbe wake unaotikisha mitandao ya kijamii kwa sasa.
Haikuwa lengo lake kufikisha ujumbe huo kwa njia ya Twitter, alipenda kufikisha ujumbe kwa Rais Magufuli moja kwa moja wakati wa uzinduzi wa maktaba mpya chuoni hapo.
Rais Magufuli alikwenda chuo hicho kufungua maktaba hiyo iliyojengwa katika Kampasi ya Mlimani (Mwalimu. Julius K. Nyerere) na kugharimu kiasi cha Sh. Bil 93.6.
Maktaba hiyo kubwa Afrika Mashariki na Kati imejengwa kwa msaada kutoka Serikali ya China na ndiyo maktaba kubwa kuliko maktaba zote ambazo China imezijenga barani Afrika.
Kwa maelezo ya Dk. Shule, mazingira ya siku hiyo yalimuashiria kusitisha mpango wake wa kupeleka ujumbe kwa muhusika (Rais Magufuli) chuoni hapo. Pia alitaka kutumia bango kuufikisha ujumbe huo.
Dk. Shule aliandika kupitia akaunti yake ya twitter “Baba @MagufuliJP umeingia Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kufungua maktaba ya kisasa. Rushwa ya ngono imekithiri mno UDSM. Nilitamani nikupokee kwa bango langu ila ulinzi wako umenifanya ninyamae. Nasubiri kusikia toka kwako maana naamini wateule wako ni waadilifu watakwambia ukweli.”
Baba @MagufuliJP umeingia Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kufungua maktaba ya kisasa. Rushwa ya ngono imekithiri mno UDSM. Nilitamani nikupokee kwa bango langu ila ulinzi wako umenifanya ninyamae. Nasubiri kusikia toka kwako maana naamini wateule wako ni waadilifu watakwambia ukweli
— Vicensia Shule (@vicensiashule) November 27, 2018
Jana Alhamis aliandika kwenye twetter: “Kwa manusura wa udhalilishaji huu wa kingono, tunakaribia kufika, tutashinda, tutapata ushindi mkubwa!
My good people, a quick update. Leo Alhamisi 29 Nov jioni nimepigiwa simu kuitwa kwenye Kamati ya Maadili siku ya Ijumaa 30 Nov mchana. Nasubiri mwaliko rasmi kwa maandishi. For our dear sexual violence survivors, we are almost there, we will win, big time! #IStandWithDrShule
— Vicensia Shule (@vicensiashule) November 29, 2018
Leave a comment