Tuesday , 3 October 2023
Home Kitengo Maisha Afya Taasisi ya Moi kuwasiliana na wagonjwa kwa simu
Afya

Taasisi ya Moi kuwasiliana na wagonjwa kwa simu

Spread the love

TAASISI ya Mifupa (MOI) imetakiwa kuanzia leo kuwasiliana na wateja wao kwa njia ya simu pale panapotokea mabadiliko ya watoa huduma kutokuwepo mahali pa kazi ilikuepusha usumbufu wa kukaa hospitalini muda mrefu. Anaripoti Khalifa Abdallah … (endelea).

Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dk. Mpoki Ulisubisya wakati alipofanya ziara katika taasisi hiyo na kukuta wagonjwa wakisubiri kwa muda mrefu kupata matibabu pamoja na vipimo.

Dk. Mpoki alisema alichokiona kwenye taasisi hiyo ni mawasiliano ambayo inasababisha wagonjwa wengi kutokupata taarifa za kutokuwepo kwa madaktari wao hivyo kufanya wagonjwa kusubiri kwa muda mrefu.

“Kuanzia leo taasisi hii itawasiliana nanyi kila inapotokea changamoto inayofanya mabadiliko ya mida yenu na madaktari, mtapigiwa simu sasa wewe utafanya maamuzi yakuja au kusubiri hadi muda ulioambiwa ili uonane na daktari wako muda utakaombiwa,” alisema Dk. Mpoki.

Aidha, aliwataka madaktari na wauguzi wawe wanawajulisha wagonjwa mapema wao kwa wale wenye simu kwani kwenye kila jarida la mgonjwa huwa wanaandika namba za simu za wateja wao.

Hata hivyo Dkt. Mpoki alisema hii ni kutokana na mkakati wa Serikali wakutatua changamoto za wananchi wanaofika kupata matibabu kwenye taasisi zake na hivyo kuboresha huduma kwa wahitaji kadri ya uwezo unavyopatikana.

Katibu Mkuu huyo alifanya ziara katika taasisi hiyo kwa kutembelea idara ya Mionzi, wagonjwa wa nje pamoja na kuongea na wagonjwa waliofika kupata matibabu katika hospitali hiyo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

AfyaHabari Mchanganyiko

Chanjo mpya ya malaria Sh 5,000-10,000

Spread the loveShirika la afya la Duniani (WHO) limeridhia chanjo ya pili...

AfyaHabari Mchanganyiko

Wagonjwa kiharusi waongezeka, Hospitali Mkapa yaja matibabu mapya

Spread the loveHOSPITALI ya Benjamini Mkapa kwa kushirikiana na madaktari Bingwa kutoka...

AfyaHabari Mchanganyiko

Wananchi Geita wachangamkia uchunguzi wa saratani bure, wanawake wapewa neno

Spread the loveMAONESHO ya Sita ya Teknolojia ya Madini Geita yameendelea kuwanufaisha...

Afya

Serikali yaanza kutekeleza maombi ya Prof. Muhongo

Spread the loveSERIKALI imeanza kutekeleza maombi ya Mbunge wa Musoma Vijijini, Prof....

error: Content is protected !!