Thursday , 2 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Serikali yaja na kibano cha AZAKI
Habari Mchanganyiko

Serikali yaja na kibano cha AZAKI

Spread the love

SERIKALI imezikemea baadhi ya asasi za Kiraia ambazo zimekuwa zikitumia vibaya fedha za ruzuku zinazotolewa na wadau mbalimbali kwa ajili ya maendeleo. Anaripoti Dany Tibason, Dodoma … (endelea).

Hayo yameelezwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. John Jingu wakati wa Ufunguzi wa wiki ya Azaki iliyofanyika kitaifa Jijini Dodoma.

Dk. Jingu ambaye alimwakilisha Waziri Mkuu Kasimu Majaliwa, alisema kuwa baadhi ya asasi ambazo zinafanya vibaya kwa kutumia fedha bila kufuata matarajio zinasababisha kuzifanya asasi nyingine zionekane hazifai.

Alisema ni muhimu zaidi kwa asasi za kiraia kuzingatia zaidi uwajibikaji na uwazi ili kuweza kuwafikia walengwa ambao wamekusudiwa kufikishiwa huduma.

Kwa upande wake Rais wa Faundation for Civil Society, (FCS), Stigma Tenga alisema kuwa asasi hiyo ambayo siyo ya Kiserikali imetoa zaidi ya Sh. 200 bilioni kwa asasi za Kiraia zaidi ya Sh. 5000 milioni katika mikoa 30 Tanzania Bara na visiwani huku zaidi watu milioni 30 wamenufaika.

Aidha Stigma alisema kwa sasa asasi za Kiraia ambazo zinafanya na FCS zinatakiwa kuzingatia utumiaji wa fedha kwa kulingana na thamani ya fedha ikiwa ni pamoja na uwazi na uwajibikaji.

Mbali na mambo mengine Stigma alisema kuwa katika kuhamikisha wanaifikia Jamii kwa urahisi FCS imefanikiwa kuwafikia watu 342,000 kwa kuwapatia matibabu bure watoto, wazee na watu ambao hawana uwezo.

Akimkaribisha Rais wa FCS, Mkurugenzi Mkuu mtendaji wa Faundation for Civil society, Francis Kiwanga alisema asasi zaidi ya 400 zimeshiriki huku washiriki zaidi ya 600 wamefika katika maonesho hayo.

Aidha alisema kuwa jukumu kubwa la maonesho ya AZAKI ni kuziwezesha assai mbalimbali kufanya vizuri huku kuweza kutanzania kazi zinazofanywa na Asasi za Kiraia kwa kushirikiana na serikali.

“Asasi za Kiraia zimekuwa zikifanya vizuri na Jamii, serikali na hususani Jamii ambazo zipo pembezoni huku ikiendelea kuhamasisha Jamii kujikita katika shughuli za kimaendeleo alisema Kiwanga.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

NEMC yatoa elimu matumizi sahihi ya zebaki kwa wachimbaji

Spread the loveBARAZA la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC)...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Oryx gesi yagawa mitungi, majiko 100 kwa waandishi wa habari Dar

Spread the loveKAMPUNI ya Oryx Gesi Tanzania imegawa mitungi 100 ya gesi...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mavunde ataja malengo “Vision 2030”

Spread the loveWAZIRI wa Madini amesema dhana ya “Vision 2030” inakusudia kuiendeleza...

Habari MchanganyikoMichezo

Wanamichezo Mei Mosi wachangia wahitaji vitu vya mil. 11.5

Spread the loveWanamichezo wanaoshiriki Michezo ya Mei Mosi Taifa 2024 jijini Arusha...

error: Content is protected !!