Saturday , 20 April 2024
Home Kitengo Maisha Elimu Prof. Ndalichako aokoa jahazi UDSM
Elimu

Prof. Ndalichako aokoa jahazi UDSM

Spread the love

PRESHA imeshuka. Ndivyo unavyoweza kusema baada ya wanafunzi 682 wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam waliofutiwa usajili kutakiwa kurejeshwa. Anaandika Regina Mkonde … (endelea).

Kauli ya kurejeshwa kwa wanafunzi hao imetolewa leo tarehe 22 Oktoba 2018 na Profesa Joyce Ndalichako, Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia.

Prof. Ndalichako ametoa kauli hiyo wakati akifungua mafunzo ya wahasibu yanayoendelea Dar es Salaam na kwamba, kauli ya kusimamishwa usajili wa wanafunzi hao aliisikia mwishoni mwa wiki iliyopita.

Prof. Ndalichako tayari ametoa maagizo kwa uongozi wa Tume ya Vyuo Vikuu (TCU) na uongozi wa UDSM kukaa na kuangalia namna ya kumaliza suala hilo bila kuathiri wanafunzi hao.

Amefafanua kwamba, UDSM kuna nafasi 3,000 na kwamba, kilichotokea ni tatizo la kiufundi kutokana na wanafunzi wengi kupenda chuo hicho.

“Wanafunzi wengi wanapenda kusoma UDSM na tatizo lilikuwa linaweza kurekebishika na wote ni idara za serikali,” amesema Prof. Ndalichako na kuongeza;

“TCU na UDSM hawakutakiwa kushindana na ndiyo maana nimewaagiza hadi Jumamosi wawe wamemaliza tofauti zao.”

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

ElimuHabari za Siasa

Walimu 52,551 kupandishwa madaraja mwaka huu

Spread the loveNaibu Waziri wa nchi, Ofisi ya Rais (Utumishi na Utawala...

BiasharaElimu

NMB yatoa vifaa vya ujenzi kwa shule sita Nyasa  

Spread the loveBENKI ya NMB imetoa msaada wa vifaa mbalimbali vya ujenzi...

ElimuHabari Mchanganyiko

GGML yawapa mbinu wanafunzi Geita Boys kufikia malengo ya kitaaluma

Spread the loveKampuni ya Geita Gold Mining Limited (GGML) imetoa mafunzo maalumu...

ElimuHabari Mchanganyiko

Wanawake GGML wawanoa wanafunzi Kalangalala Sec. kujitambua

Spread the loveKATIKA kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Wanawake Duniani, Umoja wa...

error: Content is protected !!