September 27, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Ammy Ninje Mkurugenzi wa Ufundi TFF

Ammy Ninje, Mkurugenzi wa Ufundi TFF

Spread the love

KAMATI ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), imemteuwa kocha Ammy Ninje kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Ufundi ndani ya shirikisho hilo leo Oktoba 22, 2018, na awali nafasi hiyo ilikuwa inashikiliwa na Oscar Milambo. Anaripoti Kelvin Mwaipungu … (endelea).

Ammy Ninje alishawahi kuiongoza timu ya Taifa ya Tanzania Bara Kilimanjaro Stars kwenye michuano ya CECAFA iliofanyika nchini Kenya mwaka uliopita na kuwahi kuwa kocha wa timu ya Taifa ya Tanzania chini ya umri wa miaka 20, ‘Ngorongoro Heroes.’

Bada ya kuondolewa katika nafasi hiyo Oscar Milambo ataendelea na majukumu yake kama Ofisa Maendeleo wa Vijana ndani ya shirikisho hilo na wakati huo huo kamati ya utendaji imepitisha tarehe ya mkutano mkuu ambao kisheria unatakiwa kutangazwa siku 60 kabla ya kufanyika.

Aidha kikao hicho cha Kamati ya Utendaji kimefanya mabadiliko kwenye baadhi ya kamati kutokana na baadhi ya Wajumbe kujiuzulu na wengine kukabiliwa na majukumu mengi.

Wajumbe walioteuliwa kwenye Kamati ya Nidhamu ni Kiomoni  Kibamba ambaye ni  Mwenyekiti huku wajumbe ni Peter Hella, Kassim Dau, Handley Matwenga na Twaha Mtengera. Huku Kamati ya Rufaa na Maadili itaongozwa na Richard Mbaruku ambaye ni Mwenyekiti, Makamo wake, Thadeus Karua  wajumbe ni Mussa Zungu, ASP Benedict Nyagabona na Lugano Hosea.

Kwa upande wa Kamati ya Uchaguzi wataongozwa na Mwenyekiti, Malangwe Ally huku Makamo wake akiwa Mohamed Mchengela, Benjamini Karume, Mohamed Gombati, Hamisi Zayumba.

error: Content is protected !!