Tuesday , 7 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Madereva kuwaweka kikaangoni vigogo Udart
Habari Mchanganyiko

Madereva kuwaweka kikaangoni vigogo Udart

Spread the love

WAKATI Serikali ya mkoa wa Dar es Salaam, ikiagiza watendaji wa Mradi wa Mabasi yaendayo Haraka (Udart) kutoa sababu za kutochukua hatua madhubuti kuondoa kero ya usafiri kwa abiria, ifikapo kesho majira ya saa 12.30 asubuhi, kampuni hiyo imeeleza sababu za kero hiyo. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Udart kupitia msemaji wake, Deus Bugaywa imedai sababu za kukosekana kwa usafiri kwa abiria wa Udart hasa leo tarehe 10 Oktoba 2018 majira ya asubuhi, ni mgomo wa baadhi ya madereva kwa madai ya kupinga kucheleweshewa mishahara yao.

Bugaywa ameeleza kuwa, madereva hao wameharibu mtiririko wa magari baada ya mmoja wao kwa makusudi kuziba njia ya kutokea magari hayo, kitendo kinachohujumu Udart.

“Kawaida mabasi huanza kutoka saa 9 usiku, leo yamechelewa  kuanza kazi kwa sababu kuna gari lilienda kupaki kwenye geti la nyuma ambalo mabasi yanatokea na mhusika kutokomea kusikojulikana,” amesema Bugaywa.

Kufuatia hatua hiyo, Udart inafanya uchunguzi wa hujuma hizo kwa kushirikiana na vyombo vya dola kwa ajili ya kubaini wote waliohusika, na uchunguzi utakapokamilika watachukuliwa hatua.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Mafunzo kwa bodaboda 395 yamkuna Meya Dodoma

Spread the loveNAIBU Meya wa Jiji la Dodoma, Asma Karama amepongeza mafunzo...

Habari Mchanganyiko

Samia aagiza huduma za dharura maeneo yaliyoathiriwa na kimbunga Hidaya

Spread the love   RAIS wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania, Samia...

Habari Mchanganyiko

Mahakama yatoa uamuzi zuio dhidi ya Club House

Spread the loveMAHAKAMA Kuu ya Tanzania, Masjala Kuu jijini Dar es Salaam,...

Habari Mchanganyiko

GGML, OSHA yawanoa bodaboda 200 Arusha

Spread the loveZAIDI ya madereva bodaboda 200 wa jiji la Arusha wamepatiwa...

error: Content is protected !!