Tuesday , 7 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Wahujumu miondombinu ya maji wafikia saba
Habari Mchanganyiko

Wahujumu miondombinu ya maji wafikia saba

Spread the love

BAADA ya uchunguzi  unaofanywa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) juu ya hujuma ya Maradi wa Maji wa Mtomoko uliopo katika wilaya ya Chemba na Kondoa katika mkoa wa Dodoma sasa watu saba wamefikishwa mahakamaji kwa kujibu tuhuma hizo. Anaripoti Dany Tibason, Dodoma … (endelea).

Awali watu watano juzi walifikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Dodoma wakikabiliwa na makosa kadhaa ya rushwa na uhujumu uchumi wakati wa utekelezaji wa mradi huo huku jana watu wawili wakifikishwa katika mahakama hiyo na kufanya jumla ya watuhumiwa kuwa saba.

Akizungumza na waandishi wa habari jana Jijini Dodoma, Naibu Mkuu wa Takukuru Musa Cheulo alisema kuwa kutokana na uchunguzi ulioendelea kufanyika wameweza kuwabaini watu wengine wawili ambao walihusika kuhujumu mradi huo.

“Tumeweza kuwabaini watu wengine wawili ambao wamehusika katika mradi huo natumewafikisha mahakamani watu hao ni mkurugenzi wa POA mhandisi PTE company Limited Abas Mahuna na Mhandisi wa maji halmashauri ya wilaya ya Kondoa Ali Mruma,” alisema Cheulo.

“Watu hawa wameiingizia serikali hasara ya kiasi cha Sh. 1.6 bilioni kutoka 1.4 bilioni na kusababisha ukosefu wa maji kwenye vijiji 7 za wialaya hizo,” alisema.

Hata hivyo kwa mujibu wa Cheulo alisema kuwa watuhumiwa hao hawakupewa nafasi ya kujitetea na kesi hiyo ilisikilizwa na Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Mkoa wa Dodoma, Mery Sanapere na kesi hiyo itasikilizwa tarehe 22 mwezi huu.

Awali juzi watano walikamatwa na waliokamatwa ni pamoja na mfanyabiashara maarufu wa Dodoma, Josephat Mwanshinga ambaye ni Mkurugenzi wa Kampuni ya MWANSHINGA ENTERPRISES COMPANY LIMITED iliyopewa mkataba wa kufanya kazi ya ukarabati wa Mradi wa Maji wa Ntomoko – mwaka 2014 kwa thamani ya Tsh. 2.8 bilioni.

Wengine ni Basili Mwiserya, Loini Saning’o, Lyimo Yusuph na  Hussein Modu, ambao ni wajumbe wa timu ya tathimini ya zabuni na wasimamizi wa mradi huo .

Amesema wameshtakiwa kwa makosa chini ya Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Na. 11 ya Mwaka 2007; Sheria ya Uhujumu Uchumi Sura ya 200 kama ilivyofanyiwa mapitio mwaka 2002 pamoja na Sheria ya Kuzuia Utakatishaji Fedha ya mwaka 2006.

Akitoa ufafanuzi wa  makosa hayo, awali kabla ya watu wengine kuongezeka na kufikia watuhumiwa saba, Sosthenes Kibwengo, ambaye ni Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Dodoma alisema Uchunguzi wa TAKUKURU ulibaini kuwa kwa kushindwa kutekeleza majukumu yao ipasavyo wakati wa mchakato wa zabuni na usimamizi wa mradi, washtakiwa wamekiuka sheria kadhaa na hivyo kuisababishia serikali hasara ya Tsh. 1,427,701,000.

Akiwasomea mashtaka mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Mkoa wa Dodoma, Arnold Kerikiano, Wakili Mwandamizi wa Serikali Josephat Mkizungo alisema washtakiwa wanakabiliwa na makosa ya matumizi ya nyaraka kumdanganya mwajiri, kughushi, matumizi mabaya ya madaraka, kusaidia kutenda kosa, utakatishaji wa fedha pamoja na kuisababishia serikali hasara ya kiasi hicho.

Washtakiwa hawakuruhusiwa kujibu mashtaka dhidi yao kwani mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza shauri lao, hivyo wamepelekwa rumande hadi kesi hiyo itakapotajwa tena tarehe 22 Oktoba 2018.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

AfyaHabari MchanganyikoMakala & Uchambuzi

Kisukari cha mimba ni nini?

Spread the loveKisukari cha mimba ni aina ya kisukari kinachotokea kwa baadhi...

Habari Mchanganyiko

Mafunzo kwa bodaboda 395 yamkuna Meya Dodoma

Spread the loveNAIBU Meya wa Jiji la Dodoma, Asma Karama amepongeza mafunzo...

Habari Mchanganyiko

Samia aagiza huduma za dharura maeneo yaliyoathiriwa na kimbunga Hidaya

Spread the love   RAIS wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania, Samia...

Habari Mchanganyiko

Mahakama yatoa uamuzi zuio dhidi ya Club House

Spread the loveMAHAKAMA Kuu ya Tanzania, Masjala Kuu jijini Dar es Salaam,...

error: Content is protected !!