Friday , 3 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Makonda awachongea Kubenea, Mnyika, Mdee kwa Rais Magufuli
Habari za Siasa

Makonda awachongea Kubenea, Mnyika, Mdee kwa Rais Magufuli

Spread the love

MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amelitumia Jukwaa la Uzinduzi wa Daraja la Juu (Mfugale Flyover) kumweleza Rais John Magufuli kuwa Halima Mdee, Mbunge wa Kawe, Saed Kubenea wa Ubungo na John Mnyika wa Kibamba hawaungi mkono juhudi zake. Anaripoti Faki Sosi … (endelea).

Uzindizu huo uliofanyika leo tarehe 27 Septemba, 2018 ambapo Makonda alitambulisha uwepo wa viongozi mbalimbali akiwamo Mbunge wa Temeke CUF Abdallah Mtolea na wengine wa Chama cha Mapinduzi CCM na kwamba alimueleza Rais kuwa wamefika wabunge na viongozi wa kada zote isipokuwa wabunge hao wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).

Makonda amepata kigugumizi kueleza alichokusudia baada ya kumueleza Rais kuwa wanasiasa hao hakuwakuwepo katika hafla hiyo ya uzinduzi.

”Mheshimiwa Rais ukiona yule wa Kawe hajaja, yule wa ubungo hajaja, Kibamba hajaja lakini aaah ….,” amesema Makonda bila kutoa maelezo kama walialikwa au la.

Amemtaja Mwita Waitara Mbunge wa Ukonga (CCM) kuwa yeye ndiye ishara ya kuwa CCM imekubalika kwa wananchi kutokana na ushindi wake wa asilimia 80.

Akizungumza kwenye uzinduzi huo wa daraja hilo la juu linalounganisha barabara ya Nyerere na Mandela, Makonda amesema kuwa daraja hilo litapunguza changamoto ya foleni.

Makonda amemuomba Rais Magufuli kufanya ziara katika mkoa wa Dar es Salaam kwani wamekuwa wakiona wivu sana kuona wenzao wa mikoani wanavyopata nafasi ya kuonana naye.

Amesema kwa sasa juhudi za Rais Magufuli zimewafanya WanaCCM kutembea kifua mbele tofauti na ilivyokuwa zamani kwani hapo awali waliokuwa tukivaa nguo zao walikuwa wakizomewa lakini sasa hivi wanavaa kwa kujivunia.

Wakati huo huo ameeleza mikakati yake ya kuwawezesha walemavu kupata ajira. “Tumeamua kujipanga kimkakati kuitekeza sheria inayotoa haki na usawa kwa Ulemavu. Tumejipanga ili kila muajili ajili watu waremavu” Amesema Makonda.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Chadema waendelea kulilia katiba mpya

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeendelea kudai upatikanaji wa...

Habari za SiasaTangulizi

Chadema kumshtaki Rais Samia

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimetishia kumfungulia kesi ya...

Habari za Siasa

Tume huru ya uchaguzi yatangaza uchaguzi mdogo Jimbo la Kwahani

Spread the love  TUME Huru ya Taifa ya Uchaguzi, imetangaza uchaguzi mdogo...

AfyaHabari za Siasa

Dk. Biteko aagiza utoaji huduma saratani usiwe wa kibaguzi

Spread the loveNaibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko...

error: Content is protected !!