February 24, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Cristiano Ronaldo ruksa kuivaa Man United

Spread the love

SHIRIKISHO la Mpira wa Miguu Ulaya (UEFA) limethibitisha kumfungia mchezo mmoja wa Ligi ya Mabingwa mshambuliaji wa klabu ya Juventus, Cristiano Ronaldo baada ya kuoneshewa kadi nyekundu kwenye mchezo dhidi ya Valencia. Anaripoti Kelvin Mwaipungu … (endelea).

Baada ya UEFA kutengua kadi hiyo mshambuliaji huyo ataukosa mchezo mmoja tu dhidi ya Young Boys Jumanne 2 Oktoba 2018 na hivyo atakuwa tayari kuivaa Manchester United katika mchezo wa klabu bingwa unaotarajiwa kuchezwa kwenye Uwanja wa Old Trafford Oktoba, 2018.

Ronaldo alipewa kadi hiyo baada ya kumvuta nywele mlinzi wa klabu ya Valencia, Jeison Murillo alipokuwa akimkaba na muamuzi kuamua kumchukulia hatua hizo.

error: Content is protected !!