Sunday , 28 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Waziri avunja bodi ya NSSF
Habari za Siasa

Waziri avunja bodi ya NSSF

Spread the love

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi Vijana na Ajira, Jenista Mhagama ameivunja Bodi ya Wadhamini ya Shirika la Hifadhi ya Jamii (NSSF) pamoja na kutengua uteuzi wa Mwenyekiti  na wajumbe wake. Anaripoti Mwandishi Wetu  … (endelea).

Akizungumza na wanahabari jijini Dodoma leo Julai 24, 2018 Waziri Mhagama amesema lengo la mabadiliko hayo ni kuimarisha utendaji wa NSSF.

“Lengo kuu la mabadiliko haya ni kuhakikisha  kuwa shirika linaimarishwa zaidi katika kusimamia mwenendo mzima wa kila siku wa utendaji kazi wa shirika ikiwemo kazi za msingi za kuongeza wanachama kukusanya michango kulipa mafao ya wanachama kwa wakati na kusimamia ipasavyo shughuli za vitega uchumi kwa ufamnisi na uweledi,” amesema Mhagama.

Waziri Mhagama amesema taratibu za uteuzi wabodi mpya na wajumbe wake utaendelea kufanyika kwa mujibu wa sheria.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mavunde aibana kampuni kutimiza masharti ya mkataba

Spread the loveWaziri wa Madini, Anthony Mavunde ameitaka Kampuni ya Xin Tai...

Habari za Siasa

Sauti ya Watanzania waeleza sababu za kuiunga mkono Chadema

Spread the love  KIKUNDI kinachojipambanua katika kupigania rasilimali na uhuru wa nchi,...

Habari za SiasaKimataifaTangulizi

Tanzania, Somalia kuibua maeneo mapya ya ushirikiano

Spread the love  RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amesema Tanzania na Somalia...

Habari za Siasa

ACT: Waongoza watalii wapate maslahi yao inavyostahili

Spread the loveCHAMA cha ACT-Wazalendo kimeitaka serikali kuhakikisha inasimamia maslahi stahiki ya...

error: Content is protected !!