March 4, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Kamishina wa Magereza afanya mabadiliko

Spread the love

Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza Tanzania, Phaustine Martin Kasike amefanya mabadiliko ya kiuongozi kwa wakuu wa Magereza wa mikoa na vituo nchini. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Taarifa ya mabadiliko hayo imetolewa leo tarehe 24 Julai, 2018 kwa vyombo vya habari na Mrakibu Msaidizi wa Magereza, ambaye pia ni Ofisa Habari Makao Makuu ya Jeshi la Magereza, Lucas Mboje.

Sehemu ya taarifa hiyo inaeleza kuwa, Kamishna Kasike amemhamisha Mkuu wa Magereza Mkoa wa Dodoma, Naibu Kamishna wa Magereza, DCP Julius Sang’udi kwenda Makao Makuu ya Magereza kuwa Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Wafungwa. huku nafasi yake ikichukuliwa na Mkuu wa Magereza wa Singida, Kamisha Msaidizi Mwandamizi wa Magereza, SACP Salum Hussein.

Nafasi ya SACP Hussein imechukuliwa na Kamishna Msaidizi wa Magereza, ACP Msepwa Omary aliyekuwa Mkuu wa Gereza la Mtego wa Simba. ACP Msepwa amekuwa Kaimu Mkuu wa Magereza mkoa wa Singida na nafasi yake kukaimiwa na Mrakibu wa Magereza, Muta Tibalinda.

Vile vile, taarifa hiyo inaeleza kuwa, Mkuu wa Magereza Mkoa wa Tanga Naibu Kamishna wa Magereza, DCP John Masunga amehamishiwa Makao Makuu ya Magereza kuwa Mkuu wa Kitengo cha Viwanda vya Jeshi la Magereza ambapo nafasi yake imekaimishwa kwa aliyekuwa Mnadhimu wa Magereza Mkoani Tanga, Kamishna Msaidizi wa Magereza, ACP Emmanuel Lwinga.

error: Content is protected !!