March 2, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Mkoa wako umeshika nafasi ipi maambukuzi ya VVU? Soma hapa

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu

Spread the love

TUME ya Taifa ya Kudhibiti Ukimwi (TACAIDS) imeeleza kuwa, Virusi Vinavyosababisha Ukimwi (VVU) vinaendelea kusambaa na kwamba, wananchi wanapaswa kuwa na tahadhari. Anaripoti Faki Sosi … (endelea).

Akizungumza na Wahariri wa vyombo mbalimbali ya habari Bagamoyo tarehe 24 Julai, 2018 Juma Billingi, Kamshna wa TACAIDS Mkoa wa Tanga amesema, katika utafiti wa 2016/17 inaonesha kuwa, wanawake ndio waathirika wakubwa maambukizi ya VVU.

Amesema, utafiti huo ambao unatarajiwa kutoa majibu ya jumla Septemba mwaka huu unaonesha kuwa, asilimia vijana wenye umri kianzia miaka 15-49 wanawake wameathirika kwa asilimia 6.2 huku wanaume wakiathirika kwa asilimia 3.1.

Utafiti huo unaeleza kuwa watoto wa kike wenye umri kuanzia mwaka 0-14 wameathirika kwa asilimia 0.5 huku watoto wa kiume wakiathirika kwa asilimia 0.3.

Kwenye utafiti huo watu wazima wanaume kuanzia umri wa miaka 50 na kuendelea wameathirika kwa asilimia 0.5 ambapo wanawake kuanzia umri huo wameathirika kwa asilimia 6.5.

Billingi ameeleza kuwa, utafiti huo umekuja na orodha ya mikoa na viwango vya athari ya VVU kama inavuoonekana hapa chini-: Njombe asilimia 14.8, Iringa asilimia 9.1, Mbeya asilimia 9.0, Shinyanga asilimia 7.4 Ruvuma asilimia 7.0 Dar es Salaam asilimia 6.9, Rukwa asilimia 6.2, Katavi asilimia 5.9.

Pia Pwani asilimia 5.9 Tabora asilimia 5.1,Kagera asilimia 4.8, Geita asilimia 4.7 Mara asilimia 4.5, Mtwara asilimia, Morogoro asilimia 3.8, Shinyanga asilimia 3.6, Kilimanjaro asilimi 3.8Manyara asilimia 3.2, Singida 3.3, Tanga asilimia 2.4, Dodoma, asilimia 2.9 na Lindi asilimia 2.9 , Kaskazini Pemba 0.3, Kusini Pemba asilimia 0.4 , Kaskaziniu Unguja asilimia 0.1 kusini Unguja asilimia 0.5 na Mjini Magharibi asilimia 1.4.

error: Content is protected !!