
Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo, Jenista Mhagama
WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi Vijana na Ajira, Jenista Mhagama ameivunja Bodi ya Wadhamini ya Shirika la Hifadhi ya Jamii (NSSF) pamoja na kutengua uteuzi wa Mwenyekiti na wajumbe wake. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).
Akizungumza na wanahabari jijini Dodoma leo Julai 24, 2018 Waziri Mhagama amesema lengo la mabadiliko hayo ni kuimarisha utendaji wa NSSF.
“Lengo kuu la mabadiliko haya ni kuhakikisha kuwa shirika linaimarishwa zaidi katika kusimamia mwenendo mzima wa kila siku wa utendaji kazi wa shirika ikiwemo kazi za msingi za kuongeza wanachama kukusanya michango kulipa mafao ya wanachama kwa wakati na kusimamia ipasavyo shughuli za vitega uchumi kwa ufamnisi na uweledi,” amesema Mhagama.
Waziri Mhagama amesema taratibu za uteuzi wabodi mpya na wajumbe wake utaendelea kufanyika kwa mujibu wa sheria.
More Stories
Sakata la Mahindi Kenya Vs Tanzania: Zitto aonesha njia
COVID-19: Prof. Lipumba ‘watu wana hofu’
CCM ya tetea wazawa miradi ya ujenzi