Friday , 1 March 2024
Home Kitengo Michezo Omary Kaaya Katibu mkuu mpya Yanga
Michezo

Omary Kaaya Katibu mkuu mpya Yanga

Omar Kayaa
Spread the love

KIKAO cha dharula kilichofanywa na Kamati ya Utendaji na Bodi ya Wadhamini ya Klabu ya Yanga imemteua na kumtangaza Omar Kayaa kuwa Katibu Mkuu wa muda wa klabu hiyo katika kipindi hiki cha mpito baada ya Boniface Mkwasa kujiuzulu nafasi hiyo siku chache zilizopita. Anaripoti Kelvin Mwaipungu … (endelea).

Kaaya ambaye hapo awali alikuwa meneja masoko wa klabu hiyo atashikilia nafasi hiyo kwa muda hasa katika kipindi hichi ambacho Yanga inashiriki katika michezo ya Kombe la Shirikisho Afrika na kuweka maandalizi kwa ajili ya msimu ujao wa Ligi Kuu Tanzania Bara unaotarajiwa kuanza Agosti 23, mwaka huu.

Mchezo wa marudiano kati ya Yanga na Gor Mahia unatarajiwa kuchezwa siku ya Jumapili Agosti 29, katika uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam majira ya saa moja usiku, huku Yanga ikiwa na kumbukumbu ya kupoteza katika mchezo uliopita jijini Nairobi kwa mabao 4-0.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Michezo

Wizara yaahidi kuboresha, kuimarisha michezo

Spread the loveIkiwa ni saa kadhaa baada ya kumalizika kwa mashindano ya...

Habari MchanganyikoMichezo

Nje jogging yanyakua medali 20 Kili Marathon

Spread the loveTimu ya riadha ya Wizara ya Mambo ya Nje na...

Michezo

Siku ya kukusanya maokoto ni leo, usipange kukosa

Spread the love  HATIMAYE Jumamosi imefika ndugu mteja wa Meridianbet na mechi...

Michezo

Kuwa milionea na Meridianbet ni rahisi sana

Spread the love  JE, unajua kuwa leo hii ni siku nzuri kwako...

error: Content is protected !!