Wednesday , 8 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Mtatiro wa CUF aiparura serikali ya JPM
Habari za SiasaTangulizi

Mtatiro wa CUF aiparura serikali ya JPM

Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi wa chama cha CUF, Julias Mtatiro akizungumza na waandishi wa habari
Spread the love

CHAMA cha Wananchi (CUF), kimeitahadharisha serikali kuwa mashambulizi ya demokrasia yanaweza kuleta athari kwa jamii. Anaripoti Faki Sosi … (endelea).

Hayo yameelezwa leo na Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi wa chama hicho, Julias Mtatiro alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.

Mtatiro amesema kuwa mashambulizi hayo ya vyama vya siasa yanalenga kuuwa upinzani na kubakisha chama kimoja ambacho ni Chama cha Mapinduzi (CCM).

Mtatiro ametolea mfano moja ya mashambulio hayo ni pamoja na kuzuiwa kumkosoa Rais au kulitaja jina lake.

“Kuna watu wameeelekezwa kuwa kumtaja Rais Magufulu ni dhambi, mimi mkatoliki na yeye pia anajua kuwa kumtaja siyo dhambi tutamtaja kwa sababu yeye ndiye Rais wa Jamhuri anawajibika.” amesema

Amesema kuwa shambulio lingine ni kuzuiliwa kwa vyama vya siasa kufanya shughuli zake kama ilivyoainishwa kwenye katiba.

Mtatizro amesema vyama hivyo vimewekewa vikwazo katika kufanya shughuli hizo ilhali CCM na wafuasi wake wanafanya shughuli hizo.

Amesema kuwa viongozi wa vyama vya upinzani wamekuwa wakikamatwa wanapofanya mikutano ya kisiasa ilhali Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Humphrey Polepole anafanya siasa za hadhara bila kuzuiliwa.

Mwanasiasa huyo amesema licha ya kukandamizwa kwa vyama vya siasa bado CCM inafanya biashara ya kununua madiwani na wabunge wa upinzani na kusababisha kufanyika uchaguzi mdogo ambao unagharimu fedha nyingi.

Ameleeza kuwa mbinu nyingine ni kuwafunga wanasiasa wa upinzani kwa kuwabambia kesi kama alivyofanyiwa Godbless Lema Mbunge wa Arusha Mjinia na Joseph Mbilinyi Mbunge wa Mbeya Mjini kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).

Ameongeza kuwa ukandamizaji huo wa demokrasia utaenda sambasamba na kuvibana vyombo vya habari.

Akizungumzia mhimili wa Bunge, Mtatiro ameeleza kuwa limekuwa ni kama tawi serikali jambo ambalo linasababisha kushindwa kuisimamia serikali badala yake limekosa miguu ya kusimama kama mhimili.

Amesema kwamba uchumi umezidi kuwa mbaya huku benki mbalimbali zikifungwa, mfumuko wa bei umepanda na waajiri na kampuni zinapunguza wafanyakazi.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Rais Samia ni Mzanzibari: Shida Iko Wapi?

Spread the loveTAIFA linakabiliwa na upungufu wa fikra sahihi. Upungufu huu unaonekana...

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Mpina mwiba CCM, ahofia kuzibwa mdomo

Spread the loveWAKATI Chama cha Mapinduzi (CCM), kikijinasibu kuwa kinara wa demokrasia...

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Mabeyo ametuepusha

Spread the loveNIMEGUSWA na uadilifu, utiifu na uaminifu wa Mkuu mstaafu wa...

Habari za SiasaTangulizi

CCM yaitaka TAKUKURU kuichunguza Chadema tuhuma alizoibua Lissu

Spread the loveCHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimeitaka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana...

error: Content is protected !!