Monday , 27 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Lissu aivaa serikali kuhusu Sugu
Habari za SiasaTangulizi

Lissu aivaa serikali kuhusu Sugu

Tundu Lissu, Mwanasheria Mkuu wa Chadema
Spread the love

MUDA mchache baada ya Mahakama ya Hakimu Mkazi ya Mbeya, kumhukumu kwenda jela, Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ na Emmanuel Masonga, Katibu wa Kanda ya Nyasa Chadema, Mwanasheria wa Chadema, Tundu Lissu ameivaa serikali kuhusu hukumu hiyo.

Lissu ambaye yupo nchini Ubelgiji kwa matibabu baada ya kushambuliwa kwa risasi mwaka jana, ameandika walaka wake kuhusiana na tukio hilo.

Soma waraka huo hapa chini:-

Waheshimiwa wangu salaam kutoka Ubelgiji. Nawapeni pole nyingi kwa yaliyomkuta Mh. Sugu na Goddie Masonga siku ya leo.

Naomba kuzungumzia suala hili kwa kirefu kidogo.

Kwanza, hukumu ya leo sio mwisho wa mjadala mahakamani. Bado kuna fursa, nay haki, ya rufaa High Court na, ikibidi, Court of Appeal.

Pili, hukumu ya leo haina maana Sugu atakaa gerezani muda wote huo. Kuna haki ya dhamana pending appeal. Ndivyo ambavyo tumefanya kwa viongozi na wanachama wetu wengi in the past.

Tatu, hukumu ya leo haina athari yoyote kwa ubunge wa Sugu. Katiba inaweka masharti ya kifungo cha miezi sita au zaidi, na kwa makosa ya ‘utovu wa uaminifu.’ Uchochezi au kutoa lugha ya matusi sio makosa ya utovu wa uaminifu.

Nne, pamoja na kwamba sijaona nakala ya hukumu, adhabu ya kifungo bila faini kwa kosa la kwanza ni kinyume na sentencing principles. Hii ni mojawapo ya hoja zetu zilizoshinda katika kesi ya Mh. Juakali High Court mwaka jana.

Tano, hata kama atakaa gerezani muda wote huo, hukumu za kesi za kisiasa kama hii hazijawahi kuwapunguzia heshima wapigania haki popote pale duniani.

On the contrary, kifungo cha aina hii ni beji ya heshima kwa kila mpigania haki na uhuru. Orodha ya mifano ni ndefu sana: Nyerere (ijapokuwa yeye alilipa faini), Kenyatta, Mandela, Mugabe, Fidel Castro, etc.

Alichokifanya hakimu leo ni kuwaongeza Sugu na Masonga kwenye orodha hii ya heshima. They’ll come out even bigger and stronger than when they went in.

Sita, naunga mkono pendekezo la Mh. Zitto kwamba wabunge wetu wote warekodi maneno aliyofungiwa nayo Sugu na kuyaweka mitandaoni ili watukamate na sisi pia.

Instead of agonising, let’s organise and make this issue bigger and bigger mpaka wakimbie wenyewe au watukamate na kutufunga wote.

Na sio wabunge tu, tuhamasishe kila mwanachama wetu na kila anayechukizwa na uonevu huu ayarudie maneno haya ili nao wakamatwe na kufungwa.

Tumlazimishe Magufuli na watu wake waamue: waigeuze nchi nzima kuwa gereza moja kubwa, au akubali kusemwa kwa maneno na lugha asiyoipenda. Hiyo ndio maana pekee ya freedom of speech in a democracy.

Nawatakieni kila la kheri katika hii safari ndefu ya kuelekea kwenye haki.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari MchanganyikoHabari za Siasa

Wazanzibar watarajia makubwa kutoka NMB Pesa Akaunti

Spread the loveWateja wapya wa Benki ya NMB wa Zanzibar wanatarajia neema...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Kinana aungana na Tale kugawa mitungi ya gesi 800

Spread the loveMAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara, Abdulrahman...

Habari za SiasaTangulizi

Makonda amjibu Mwenyekiti UWT, “wananipa nguvu ya kuwapiga spana”

Spread the loveMKUU wa Mkoa wa Arusha, Paul Makonda amemshukia Mwenyekiti wa...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Madeni ya bilioni 219 yalipwa, wadai wengine waitwa

Spread the loveSERIKALI imesema kuanzia Mei mwaka 2021 hadi sasa imelipa madai...

error: Content is protected !!